Nchi ‘isiyotambuliwa’ duniani kumchagua Rais leo

Raia wa Somaliland wanapiga kura leo Novemba 13, 2024 kumchagua Rais wa nchi hiyo ikiwa ni uchaguzi wa nne tangu kuanzishwa kwa uchaguzi huru na haki.

Licha ya nchi hiyo kujitangazia uhuru wake tangu mwaka 1991 baada ya kuvunjika kwa iliyokuwa Serikali ya Somalia kipindi hicho, bado haijulikani kama nchi katika duru za kimataifa.

Watu zaidi ya milioni moja wanatarajiwa kupiga kura katika vituo 2,000 vya kupigia kura, huku zaidi ya waangalizi wa kimataifa 28 wapo kufuatilia mwenendo wa uchaguzi huo.

Rais Muse Bihi Abdi aliyepo madarakani anatetea kiti chake kwa muhula mwingine wa pili kupitia chama chake cha Kulmiye.

Tangu Taifa hilo lipate uhuru kutoka Somalia, Somaliland imefanikiwa kuunda Serikali yake, fedha, ulinzi na usalama wa nchi hiyo licha ya kutotambuliwa duniani.

Kutokana na changamoto za kiuchumi imesababisha kuchelewa kufanyika uchaguzi tangu mwaka 2022, hivyo unafanyika leo Novemba 13, 2024.

Related Posts