Polisi wachunguza tukio la uhalifu

 

JESHI la Polisi nchini limesema, linachunguza tukio la picha mjongeo iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii siku ya jana, ikionesha watu ambao wakijaribu kumkamata na kumuingiza kwenye gari ndogo kwa kutumia nguvu Deogratius Tarimo, mfanyabiashara anayeishi Kibaha Mkoa Pwani. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Katika taarifa yao waliyoitoa hii leo tarehe 13 Novemba 2024, Polisi imeeleza kuwa, tukio hilo lilripotowa na Deogratius mwenyewe tarehe 11 Novemba 2024, katika kituo cha Polisi Gogoni jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo lilitokea kwenye Hotel ya Rovenpic, iliyopo eneo la Kiluvya, ambapo kwa mujibu wa maelezo ya jeshi la polisi limesema kuwa sababu za kibiashara ndizo zimepelekea kutokea kwa tukio hilo, kama ilivyoelezwa na Deogratius mwenyewe wakati akiripoti tukio hilo kwenye kituo cha Polisi Gogoni.

Kwa mujibu wa maelezo ya Polisi mara baada ya kumuhoji muhusika kituo hapo wemesema kuwa, Deogratius alikuwa akufanya mawasiliano na watu hao toka tarehe 25 Oktoba 2024, kuhusu kutaka kufanyanao biashara ambayo hawakuiweka wazi.

Aidha jeshi hilo limeuhakikishia Umma kwamba, litahakikisha kinawamakat wao hao ambao walijaribu kufanya tukio hilo, kama ilivyoonekana kwenye picha zilizosambaa mtandaoni, kulingana na ushahidi ambao umeshakusanywa na unaoendelea kukusanywa.

Katika picha hizo ambazo zimesambaa, zilionesha Deogratius alifanikiwa kuwazidi nguvu watu hao watatu ambao walijaribu kutaka kumuingiza kwenye gari, huku akipiga kelele za kuomba msaada kwa watu na akitamka maneno ya kwamba “Wanakwenda kuniua, nisaidieni.”

About The Author

Related Posts