TIRA kutoa taarifa ya utendaji wa soko la Bima Nov 22

 

MAMLAKA ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) inatarajia kutoa taarifa ya utendaji wa soko la Bima tarehe 22 Novemba 2024, kwenye ukumbi wa Superdom Masaki jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Akizunguma na waandishi wa habari leo tarehe 13 Novemba 2024, Kamishna wa Mamlaka hiyo Dk. Baghayo Saqware alipokuwa anatoa taarifa juu ya uzinduzi wa taarifa hiyo.

Dk. Saqware amesema kuwa kwenye taarifa hiyo kutakuwa na mijadala itakayoeleza umuhimu wa Bima kwa wananchi pamoja na mjadala wa Bima ya afya kwa wote itakayosimamiwa na TIRA kuanzia mwaka ujao.

“Itakapofika 22 novemba tira itatoa taarifa ya utendaji wa soko la bima nchini katika ukumbi wa superwoman Dar es Salaam” amesema Dk. Saqware

Amesema kuwa umuhimu wa bima hiyo ni pamoja na kuwaepusha wananchi na umasikini baada ya kupata majanga.

“Umuhimu wa bima kwa wananchi bima ni bidhaa au huduma inayotoa kinga kwa Mali, afya na uwekezaji nyinyi ni mashahidi kwamba bidhaa za bimaa zilivyowasaidia wananchi kuepukana na umasikini ukiwa na bima mwananchi hawezi kupata umasikini kwa sababu fidia ya bima” amesema Dk. Saqware .

Dk. Saqware amesema kuwa wananchi wanapaswa kujua umuhimu wa kuweka kinga ya bima “watu hawajapata taarifa sahihi juu ya Bima mfano watu wanarudi kwenye umasikini baada ya kuunguliwa na nyumba ikiwa thamani ya bima ya Nyuma ni asilimia moja ya thamani ya gharama zote za nyuma”

About The Author

Related Posts