FIBA yatoa mipira 10 ya 3×3

SHIRIKISHO la Mpira wa Kikapu la Kimataifa (FIBA), limetoa mipira 10 kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huo wa 3×3 unaohusisha wachezaji wanne, huku wa tatu wakiwa wanacheza ndani ya uwanja na mmoja wa akiba.

Kamishna wa ufundi wa makocha wa shirikisho la mchezo wa kikapu nchini (TBF), Robert Manyerere alisema baada ya kupokea mipira hiyo waligawa kwa wasimamizi wa mchezo huo, katika mikoa ya Morogoro, Mwanza, Mbeya, Arusha, Dar es Salaam na Unguja.

Wakati huohuo, mashindano ya vyuo vya Tanzania ya 3×3 yatafanyika Desemba mwaka huu na yalikuwa yafanyike kwenye Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Novemba mwaka huu, kabla ya kuahirishwa kupisha Ligi ya Kikapu la Taifa (NBL) inayoendelea mkoani Dodoma.

Alisema baada ya kufanyika mashindano hayo, wanakusudia kuandaa pia ya vyuo vikuu vya Afrika mashariki na kati.

Related Posts