Ilikuwa robo fainali ya kibabe NBL

DAR City, UDSM Outsiders, ABC na Kisasa Heroes zimetinga nusu fainali ya Ligi ya Kikapu ya Taifa (NBL), baada ya kushinda hatua ya robo fainali kwenye Uwanja wa Chinangali, Dodoma.

Kisasa ya Dodoma ilitinga hatua hiyo baada ya kuifunga JKT ya Dar es Salaam kwa pointi 61-52, huku UDSM Outsiders (DSM) ikiichapa Eagles ya Mwanza kwa pointi 90-57.

ABC ya Dar es Salaam iliifunga Mvumi Ripper ya Dodoma kwa pointi 84-58, huku Dar City ya Dar es Salaam nayo ikiichapa TBT kwa pointi 123-37 na robo ya kwanza Dar City ilianza kwa kasi na kuonyesha ilidhamiria kufanya maangamizi makubwa, kushinda robo zote nne kwa pointi 31-13, 41-6, 20-10 na 31-8.

Akiongea na Mwanaspoti kwa simu kutoka Dodoma, kocha wa kikapu wa TBT, Aq Qassim Anasi alisema licha ya kipigo walichokipata, lakini malengo waliojiwekea ni kuhakikisha wanacheza ligi hiyo.

“Tumekuwa tukicheza mashindano ya kawaida kama yale yanayochezwa katika kituo cha Jakaya Mrisho Kikwete,” alisema Anasi.

Related Posts