Mkurugenzi wa Operesheni wa Fild guide Association of East Africa, Herbeth Madai akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 14, 2024 katika kongamano la wadau wa Utalii wa Buluu na Kijani.
Afisa Uwekezaji Mwandamizi Kituo hicho, Nestory Kissima, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 14, 2024 katika kongamano la wadau wa Utalii wa Buluu na Kijani.
SERIKALI imeombwa kutoa serikali mwelekeo wake kwaajili ya Wadau wa Utalii wa Kijani na wa Buluu kwani Tanzania imekuwa ikitangaza sana utalii wa Kijani na sio maeneo ya utalii wa Buluu.
Hayo yamesemwa na Mwenyeki wa Tanzania Umoja wa Watalii Tanzania (TCT), Moustafa Khatawa wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Novemba 14, 2024 katika kongamano la wadau wa Utalii wa Buluu na Kijani.
Amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kuangalia namna ya kushirikiana kati ya serikali na sekta binafsi, pia kuwa na ushirikiano mhimu ambao utasaidia kukuza sekta ya Utalii nchini.
Amesema serikali imekuwa ikitangaza sana maeneo ya maeneo mengine lakini sio maeneo ya mwambao wa pwani ya bahari ambayo ni Tanga, Bagamoyo, Kusini Kilwa, Mikindani na Mafia ambapo kunafursa nyingi za utalii wa bahari na Uvuvi katika Maeneo hayo.
Amesema ukanda wa Bahari unakilomita 1400 lakini maeneo mengi bado hayajatangazwa kwaajili ya utalii pamoja na fursa ya Uvuvi.
“Kongamano hili litazungumzia changamoto ambazo wanazipata sekta binafsi na wadau katika uchumi wa buluu katika ukanda wa Pwani na uchumi wa Kijani katika nchi kavu.”
Amesema kuwa kwenye kongamano hilo kutakuwa na mada mbalimbali, mazungumzo na wenzetu wa Utalii na kutoka serikalini ili kupata muafaka maalumu na kutoa mapendekezo na nini kifanyike mwishoni wa kongamano.
“Tunafutahi viongozi kutoka serikali wapo hapa ambao ni kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), wapo hapa kutoa mwelekeo wa kutoka taasisi zao kuhusu changamoto watu wa Utalii wanazozipata.
Kwa upande wa Mkuu wa Kitengo cha uthamini wa Miradi kutoka Kituo cha Ubia baina ya sekta ya Umma na Binafsi( PPPC), Dkt Suleiman Kiula amesema kuwa serikali imejidhatiti kutengeneza sheria bora kati ya sekta binafsi na sekta ya umma.
“Kwa maboresho ya sheria ambayo yamefanyika mwaka huu naamini kwamba yataiweka nchi yetu katika nafasi nzuri ya kuhamasisha ushirikiano kati ya sekta ya binafsi na sekta ya umma.”
“Kunamaeneo mhimu ambayo tumeigusa sheria na tunaamini kwa kuanzisha kituo hiki cha ubia ambachacho kimeanza rasmi mwaka huu Aprili, 2024 tumekuwa tukipokea maombi mengi ya kushirikiana na sekta binafsi, na sisi kituo cha ubia Mkurugenzi wetu, David Kafulila amekuwa amekua akifanya uhamasishaji wa mara kwa mara na kuratibu baina ya sekta binafsi na taasisi za kiserikali katika ile miradi ya kipaumbele ambayo nchi yetu imeitazama katika kufikia malenvo yake ya uchumi endelevu, na tukizingatia sasa hivi tupo katika mchakato wa kutengeneza ‘Vision’ ya maendeleo ya mwaka 2050.” Ameeleza Kiula
Amesema jambo kubwa ambalo limesisitizwa katika ‘Vision’ ya 2050 ni namna gani tunaweza kushirikisha sekta binafsi katika kutekeleza miradi ya maendeleo ya serikali ambayo inaaaminika ndio mtindo unakubalika katika kujipatia maendeleo.
Amesema katika mkutano wa Sekta ya Utalii wa Kijani na Buluu kwa maana kwamba wanaangali umhimu ambao umejificha katika utalii wa Kijani ambapo kuna utalii wa mbuga za wanyama na vivutio vingine, lakini Uchumi wa Buluu ni katika bahari na utalii wa bahari na vyote vilivyomo baharini pamoja na Uvuvi.
Amesema kuwa sekta binafsi inashika nafasi yake katika ubia ambapo kunakuwa na mradi ulioanzishwa na serikali au sekta binafsi serikali huwa huchukua asilimia 25 tuu ya ubia ili sekta binafsi ichukue nafasi kubwa ili kuleya ufanisi katika mradi.
Akizungumzia namna Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Afisa Uwekezaji Mwandamizi Kituo hicho, Nestory Kissima, amesema kuwa TIC imejikita katika kutangaza Uwekezaji uliopo katika sekta ya Utalii na uchumi wa Kijani na Buluu.
Amesema kuwa Mkutano wa leo umewapa mambo mhimu ambayo yatawawezesha kuangalia fursa zilizopo katika sekta ya utalii wa Kijani na Buluu.
Amesema kuwa TIC inapata nafasi ya kuwasilisha juu ya fursa zilizopo katika upande wa Pwani ni Hoteli, fursa zilizopo kwenye Maji, utalii wa Chini ya Maji kwamaana ya kuangalia samaki lakini pia wanazofursa za Utalii katika upande wa Utalii wa Kijani ambazo ni Mambo ya kihistoria, ujenzi wa Mahoteli pamoja na mnyororo wa thamani wa Utalii.
Kwa Upande wa Mkurugenzi wa Operesheni wa Fild guide Association of East Africa, Herbeth Madai ameiomba serikali kuwe na viwango sawa vya kuongoza watalii katika nchi za Afrika Mashariki.
“Tuweze kutengeneza mfumo ambao utakuwa unaviwango vinavyotambulika Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda hivi vitapelekea utendaji wa kazi uwe mzuri kwa maendeleo endelevu.”
Amesema kuwa waendesha utalii wasiwe wanafanya kazi bila kufuata muongozo au maadili ya uongozaji watalii pia itasaidia katika uhifadhi wa mazingira.