MENEJIMENTI YA LRCT YAHIMIZWA KUWA NA MIKAKATI MADHUBUTI YA KUSIMAMIA MABADILIKO YAO

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi akizungumza na watumishi wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania leo Novemba 14,2024 Jijini Dodoma kwenye mkutano wa 21 wa Baraza la wafanyakazi wa tume hiyo.

Katibu mtendaji wa tume ya kurekebisha sheria George Mandepo akizungumza na wafanyakazi wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania leo Novemba 14,2024 Jijini Dodoma kwenye mkutano wa 21 wa Baraza la wafanyakazi la tume hiyo.

Naibu Katibu Mtendaji LRCT Bi. Zainabu Chanzi akizungumza na wafanyakazi wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania leo Novemba 14,2024 Jijini Dodoma kwenye mkutano wa 21 wa Baraza la wafanyakazi la tume hiyo.

Mwenyekiti wa  LRCT Jaji Winifrida Karosso akizungumza na wafanyakazi wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania leo Novemba 14,2024 Jijini Dodoma kwenye mkutano wa 21 wa Baraza la wafanyakazi la tume hiyo.

Baadhi ya wafanyakazi wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania waliohudhuria leo Novemba 14,2024 Jijini Dodoma kwenye mkutano wa 21 wa Baraza la wafanyakazi la tume hiyo.

Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Tume ya kurekebisha sheria Tanzania na Waziri wa Katiba na Sheria Prof.  Palamagamba Kabudi kwenye mkutano wa 21 wa Baraza la wafanyakazi la tume hiyo.

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Waziri wa Katiba na Sheria Prof. Palamagamba Kabudi ameisihi Menejimenti ya Tume ya kurekebisha sheria Tanzania (LRCT), kuendelea kuwa na mikakati madhubuti ya kusimamia mabadiliko ya tume kwa karibu na kufanya mawasiliano na watumishi wote wakati wa utekelezaji ili kuwe na kipindi cha mpito chepesi cha utekelezaji wake.

Prof. Kabudi ameyasema hayo leo Novemba 14,2024 Jijini Dodoma wakati akifungua mkutano wa 21 wa Baraza la wafanyakazi wa tume ya kurekebisha sheria Tanzania.

“Kwahiyo naamini mada itakayotolewa leo iwe ni mrejesho mzuri na wa hakika hivyo wote tuzingatie na kutekeleza mtakayoambiwa na kushauriana,”amesema.

Aidha Prof. Kabudi amesema ni muhimu sheria zinapotungwa kwaajili ya kukabiliana na matatizo na changamoto zinazojitokeza kuwa zimefanyiwa utafiti wa kina ili kuzifanya kuwa bora na endelevu.

“Ni muhimu sheria zinapotungwa kwaajili ya kukabiliana na matatizo na changamoto zinazojitokeza kuwa zimefanyiwa utafiti wa kina ili kuzifanya kuwa bora na endelevu na tafiti hizi zinasaidia sheria kuhakisi na kukidhi mahitaji ya kutungwa kwake,”amesema.

Pia amewakumbusha kuanza maandalizi ya kuelekea kustaafu na maandalizi huanza pale mtumishi anapokabidhiwa barua ya kuanza ajira yake ya kwanza kwani ni moja kati ya viambatanishi vinavyohitajika pale mtumishi anapojaza fomu ya kuomba kustaafu.

“Sasa ni lazima uanze kujiandaa ili kuhakikisha maisha yako ya ustaafu ni ya amani, furaha na heshima baada ya kustaafu, na hakuna kitu kigumu sana uzeeni unaanza kuwa omba omba au unakuwa bugdha kwa watoto wako unaomba hela,”amesema Prof. Kabudi.

Akizungumzia suala la usalama kwa watu wanaotoa taarifa zinazosaidia vyombo vya sheria Katibu mtendaji wa tume ya kurekebisha sheria George Mandepo amesema tayari wamefanya utafiti wa namna ya kuweza kuwalinda.

“Mambo ambayo tumebaini ni kuwa mfumo wa sheria ulikuwa na mianya ya watu kuweza kuwasilisha kwanza ile taarifa lakini ni wapi watu wawasilishe na wakishawasilisha nani anaweza kusimamia haki au kumlinda yule mtoa taarifa iliabaki salama na taarifa zake zisiweze kutoka,”amesema.

Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Wafanyakazi nchini (TULGHE), Rugemalira Rutatina amesema ni wajibu wa wafanyakazi kuhakikisha wanatimiza wajibu wao na katika baraza hilo yanajadiliwa mambo mbalimbali na sio suala la maslahi pekee.

Related Posts