Mikopo nyonyaji inayowatesa wananchi Kibaha,watoa ya moyoni kukimbia familia usiku

Wananchi wa halmashauri ya wilaya ya Kibaha wa.eishukuru serikali kurudisha mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na serikali bila kuwa na riba kwani waliteseka kwa zaidi ya miezi 19 hali iliyowapelekea kuingia katika mikopo yenye riba kubwa inayotolewa mitaani maarufu kama Kaush Damu.

Hayo wameyasema wakati wa halfa ya utowaji wa mala ya kwanza kwa baadhi ya vikundi ambavyo vimepokea zaidi ya milioni 89 kati ya milion 893 zilizotengwa na halmashauri kwa ajili ya kuwakopesha wananchi.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya jamii wa halmashauri ya kibaha Shukuru Lusanjara amesema kwa sasa umewekwa utaratibu mpya wa watu kupata ambapo hata umri wa vijana umeongezwa mpaka kufikia miaka 45 kutoka zamani mwisho ilikua miaka 35 hukuakisema kama serikali wametenga milioni 893 kuwakopesha vikundi hivyo wachangamkie fursa hiyo kwa kufata vigezo kwa afisa maendeleo ya jamii ngazi ya kata watapata utaratibu wote na sio lazima kufika wilayani.

Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la kibaha vijijini amesewataka wananchi kukopa fedha hizo na kufanyiwa malengo yaliyopangwa na kuacha kutumia kwa matumizi ambayo si ya lazima kwani ni sehemu ya chanzo cha kutorudishwa mikopo.

Aidha ameongeza kua anashukuru mikopo hiyo kurudi kwani itawasaidia zaidi wananchi kuepukana na mikopo chechefu kwani imesababisha ndoa kuvunjika lakini pia kuwapa umaskini pia.

 

 

Related Posts