Mwanamke akutwa na nyaraka feki ya kifo cha mwenye eneo Bunju,waziri aagiza akamatwe

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Deogratius Ndejembi amemrejeshea Bw. Daudi Mfangavo kiwanja namba 23 kitalu 15 Mbweni Mpiji, Dar es Salaam ambaye alidaiwa kufariki dunia.

Mhe Ndejembi ameto agizo la kuchukuliwa hatua Bi Nuru Mandela aliyefoji nyaraka zinazoonesha kuwa yeye ndie Mke halali wa Bw. Mfungavo ambaye alidai alifariki dunia Juni 2011 na kukiuza kwa Bw. Mfungavo ambaye alidai alifariki dunia Juni 2011 na kukiuza kwa Bw. Servas Mkomba baada ya kupata hatimiliki ya kiwanja hicho.

“ Huu ni mtandao mkubwa hivyo namuelekeza Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi kuwachukulia hatua kali watumishi wote watakaobainika kuhusika na uuzaji wa kiwanja hiki kwa njia ambazo sio halali ili iwe mfano kwa Watumishi wote ambao wamekua wakihusika na matukio kama haya ili kuweza kurudisha uadilifu kwenye Wizara hii.

Lakini pia vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kupitia kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni navyo vifuatilie kwa wenzake wote walioshiriiana na Nuru ili waweze kufikishwa katika vyombo vya kisheria ili kuweza kutokomeza mtandao huu wa kitapeli,” Amesema Mhe Ndejembi.

Aidha Mhe Ndejembi ameelekeza kufutwa kwa hati ya mwanzo iliyotolewa kwa aliyekua mnunuzi wa kiwanja hicho na badala yake Bw. Mfangavo aweze kupatiwa hati yake halali ndani ya saa 24.

 

Related Posts