OCEAN ROAD WAWAOKOA WANAWAKE 12 WALIOKUWA HATARINI DHIDI YA SARATANI SHINGO YA KIZAZI MKOANI DODOMA

Na Mwandishi Wetu

MADAKTARI Bingwa wa Taasisi ya Saratani ya OCEAN ROAD kupitia huduma ya MKOBA ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wamefanikiwa kuokoa wanawake 12 mkoani Dodoma waliokuwa hatarini dhidi ya Saratani ya shingo ya Kizazi.

Pia wataalamu hao wameungana na wataalamu wa hospitali mbalimbali za binafsi na serikali katika kutoa huduma za uchunguzi na matibabu mkoani humo huku wakisisitiza hatari ya matumizi ya shisha kupita kiasi.

Akizungumza mkoani Dodoma Meneja Huduma za Uchunguzi na Elimu kwa Umma Dkt.Maguha Stephano,amesema wamefanikiwa kuokoa maisha ya wanawake 12 dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi Wilayani Kondoa.

“Kupitia huduma hii ya MKOBA ya Rais Dkt Samia, tukiwa katika hatua za uchunguzi wanawaje 12 wa halmashauri ya Wilaya ya Kondoa wamegundulika kuwa na viashiria vya awali vya saratani ya mlango wa kizazi hivyo tumewahi matibabu na kinga ,”amesema

Ameongeza kuwa akina mama hao wamepatiwa tiba ya viashiria hivyo na kuwa kinga dhidi ya saratani hiyo hivyo wanajivunia kunusuru maisha yao.

Dkt. Maguha amesema pia wameungana na hospitali na taasisi za serikali na binafsi katika kuadhimisha wiki ya magonjwa yasiyo ya kuambukiza Mkoani humo kwa kufanya uchunguzi dhidi ya saratani.

Amesema huduma hizo zinatolewa bure viwanja vya Nyerere “squre”.

“Nihimize wananchi kufanya uchunguzi wa saratani hasa wakina baba ambao kwa sasa kuna ongezeko kubwa la saratani ya tezi dune, waondoe hofu tunafanyaje uchunguzi kwa njia ya damu na kwa tezi dume tunapima wale wa kuanzia miaka 50 ambao wapo hatarini.

“Pia nikumbushe wananchi kuepuka matumizi ya shisha ambayo yameongezeka sana, pombe kupita kiasi,kula milo isiyo bora na kufanya mazoezi kuepuka magonjwa haya,”ameissitiza.



Related Posts