RAIS SAMIA AVUNJA REKODI KUSHIRIKI MKUTANO WA G20

 

Rais Samia Suluhu Hassan amealikwa kushiriki mkutano wa viongozi wa G20 utakaofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil kuanzia Novemba 18 hadi 19, 2024 ukiwa na kauli mbiu  inayosema ‘Kujenga ulimwengu wa haki na sayari endelevu’. 

Mwaliko huo umetolewa na Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil ambapo Rais Samia atakuwa ni  Rais wa kwanza  mwanamke kuwahi kuhudhuria mkutano wa viongozi wa G20 na Rais wa kwanza wa Tanzania kuhudhuria mkutano huo wa viongozi wa G20 tangu kupanuka kwa kundi hilo kutoka G8 hadi G20 mwaka 2009. 

Ushiriki wa Rais Samia katika mkutano wa viongozi wa G20 unaashiria kuongezeka kwa ushawishi na mwonekano wa Tanzania katika jukwaa la kimataifa na ukuaji wa diplomasia na sera za uwekezaji nje ya mipaka ya Tanzania. 

G20 inajumuisha  nchi 19 ambazo ni Argentina, Australia, Brazil, Canada, China, Ufaransa, Ujerumani, India, Indonesia, Italia, Japan, Jamhuri ya Korea, Mexico, Urusi, Saudi Arabia, Afrika Kusini, Uturuki, Uingereza na Marekani pamoja na mashirika mawili ya kikanda ambayo ni Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa  Afrika (AU) hadi mwaka 2023

Sifa mojawapo ya nchi wanachama wa G20 ni kwamba zinawakilisha takribani asilimia 85 ya Pato la kimataifa,  zaidi ya  asilimia 75  ya biashara za kimataifa na karibu theluthi mbili ya watu duniani hii ni fursa kubwa ya kufungua milango ya uwekezaji kwa Tanzania. 

Kila la heri Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Related Posts