Vyama vya Siasa waeleza mchakato wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za uchaguzi Tanga

Katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika tarehe 27/11/2024 Viongozi wa vyama vya siasa Mkoa na Wilaya ya Tanga wamefanya mkutano na waandishi wa habari lengo likiwa ni kujadili zoezi la uteuzi wa wagombea na ushirikishwaji wa vyama hivyo.

Wakizungumza wakati wa mkutano huo viongozi hao wameweza kubainisha namna hali ilivyo katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zilizopo kuweza kufikia lengo walilojiwekea katika kutekeleza zoezi la uchaguzi huo.

Hata hivyo viongozi hao wamempongeza Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Mkuu wa Wilaya ya Tanga na wasimamizi wa uchaguzi ngazi ya wilaya kwa ushirikiano walioutoa katika kufanikisha zoezi hilo la uchaguzi na kuwaomba waendelee kutoa ushirikiano huo ili kufanya uchaguzi wa uhuru na haki.

Related Posts