Wanaume Iringa ruksa kwa macho yao kushuhudia wake zao wakijifungua – Hosp ya rufaa mkoa

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa IRRH Imeanza Rasmi kutoa huduma ya Kujifungua ukiwa na msaidizi yaani mama , mwenza au rafiki kama mwomgozo wa ” Chati uchungu” iliyotolewa na Wizara ya Afya inavyosema ambapo Sasa mume anaweza kuruhusiwa kumuona mkewe akijifungua na huduma hii ni ya kwanza kutolewa mkoani Iringa Kwa Hospitali za Umma.

Maboresho Hayo yamefanywa Ili kumuwezesha mama mjamzito kupata huduma Bora zaidi na kuwa karibu na msaidizi wake au mwenza wake .

AyoTv imezungumza na Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa IRRH Alfred Mwakalebela Amesema huduma hiyo ni mpya Kwa Mkoa wa Iringa na imeshaanza kazi ambapo ameendelea kusema huduma hiyo inamsaidia mama kupunguza uchungu na kujiona hajatengwa na Mama Mjamzito ndiyo anachagua nani aambatane naye wakati wa uchungu mpaka wakati wa kujifungua

” Majukumu ambayo Mtu wa karibu wa mtu aliyekuja Kujifungua anapewa ni pamoja na kumliwaza mtu anayejifungua , kwa kupiga nae story pamoja na kumpapasa mgongoni kwasababu uchungu unapungua kidogo ” Alfred Mwakalebela

Hata hivyo AyoTv imezungumza na watu mbalimbali kuhusiana na huduma hii kuanzia ambapo wamesema huduma hii itasaidia kudumisha upendo kwenye familia

Related Posts