WAZIRI LUKUVI AELEZA MAONO YA ISIMANI IJAYO

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akizungumza na wananchi katika mikutano tofauti katika ziara yake kata Kising’a Tarafa ya Isimani Mkoani Iringa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akisalimiana na wananchi wakati wa ziara yake ya kikazi katika kijiji cha Igingilanyi katika kata ya Kising’a Mkoani Iringa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani akiteta jambo na Mhe. Rita Mlagala wakati wa ziara yake ya kikazi katika Jimbo la Isimani Mkoani Iringa.

Mwandishi wetu.

IMEELEZWA kwamba mpango wa kuchimba mabwawa ya kuhifadhi maji kwa ajili ya matumizi ya shughuli za kilimo kwa wananchi wa Tarafa ya Isimani utachangia kukuza fursa za uchumi na kuimarisha kipato cha wananchi.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi (Mb) Isimani wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo la isimani Katika Kata ya Kising’a leo tarehe 13/11/2024.

Amefafanua kwamba miradi ya maji safi imefanikiwa kutokana na fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kusaidia kupatikana maji kutoka chanzo cha maji Kilolo na Maji kutoka Mtandao wa Maji Iringa Mjini kupitia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mjini Iringa (IRUWASA).

“Lazima tufikirie namna ya kuweka mipango ya kuhifadhi maji ili yatusaidie katika shughuliza kilimo cha umwagiliaji na yasaidie mwananchi mmoja mmoja katika kuimarisha uchumi wa wananchi wa Isimani,” alisema Waziri Lukuvi.

Ikiwa huduma zote muhimu za Maji, Barabara, Elimu, Afya Serikali imeimarisha sasa ni wakati wa kufikiria mipango endelevu itakayosaidia wananchi kuhifadhi maji ili kukabilina na hali ya ukame.

Kwa Upande wake Diwani wa kata ya Kising’a Mhe.Rita Mlagala ameishukuru Serikali kupitia Halmashauri ya Iringa kwa kutenga kiasi kikubwa cha fedha katika mikopo ya asilimia kumi inayotolewa kwa ajili ya Vijana Wanawake na Makundi maalumu.

Mhe. Mlagala amesema,”fedha hizo zitagawawiwa kwa usimamizi mzuri kwa kuangalia vikundi vienye sifa kwa kupitia utaratibu uliowekwa na serikali wa kuwa na Kamati za Mikopo za Kata zitakazo ratibu utoaji wa mikopo hiyo.”

Related Posts