JK KATIKA SHUGHULI YA KUAGA MWILI WA MAREHEMU LAWRENCE MAFURU

RAIS Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoa mkono wa pole kwa wafiwa wakati wa kuaga mwili wa aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Marehemu Lawrence Nyasebwa Mafuru katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam Alhamisi tarehe 14 Novemba, 2024.

Mhe. Dkt. Kikwete alifika hapo akitokea Uwanja wa Ndege moja kwa moja akitokea kuhudhuria vikao vya Bodi ya Taasisi ya Kimataifa inayoshughulikia masuala ya Elimu Duniani (GPE), ambayo yeye ni Mwenyekiti wake, jijini Washington DC, Marekani.

Related Posts