Kwaheri Christina Kibiki – Balozi Dkt Nchimbi aongoza maelfu ya waombolezaji

Maelfu ya waombolezaji , pamoja na viongozi mbalimbali wa Vyama pamoja na serikali wamefika katika ibada ya mazishi ya kumuaga aliyekuwa katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kilolo ambaye hivi karibuni alifariki dunia baada ya kushambuliwa ka risasi na watu ambao bado hawajafahamika

Maelfu ya watu hawa yameongozwa na Katibu mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Balozi Dkt John Nchimbi , Pamoja na viongozi wengine Akiwemo pia mwenyekiti wa Wanawake UWT Marry Chatanda

Ndugu Kibiki alipoteza uhai usiku wa tarehe 12 Novemba 2024, katika tukio hilo la kikatili, baada ya kuvamiwa na kupigwa risasi akiwa nyumbani kwake usiku huo, ambapo hadi sasa wahusika wa unyama huo bado hawajajulikana, huku vyombo vya dola, kupitia jeshi la polisi, vikiendelea kuwasaka kwa ajili ya hatua za kisheria.

Related Posts