Rais Samia amlilia King Kikii

 Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Rais wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kutokana na kifo cha mkongwe wa muziki wa dansi, Boniface Kikumbi ‘King Kikii’ na kusema nguli huyo atakumbukwa na kuenziwa kwa kazi zake nyingi nzuri ikiwamo wimbo wa kitambaa cheupe.

Amesema King Kikii ametoa burudani kwa mamilioni ya Watanzania na amekuwa mlezi na mwalimu wa wengi katika tasnia ya muziki.

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

“Ninatoa salamu za pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki, wasanii na wapenzi wote wa muziki nchini kufuatia kifo cha mwanamuziki nguli Boniface Kikumbi Mwanza Mpango ‘King Kikii’.

Kwa zaidi ya miaka 50 King Kikii. Tutamkumbuka na kumuenzi kwa kazi zake nyingi na nzuri ikiwemo wimbo wake maarufu wa ‘Kitambaa Cheupe’ ambao umeendelea kuwa sehemu ya burudani kwenye maeneo na shughuli mbalimbali za burudani nchini.

“Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema”

King Kikii amefariki usiku wa kuamkia leo Novemba 15, 2024 nyumbani kwake Mtoni kwa Aziz Ally, jijini Dar es Salaam.

Related Posts