TIA MTWARA YAFANYA MAHAFALI YA 22, WAHITIMU WATAKIWA KUTUMIA ELIMU WALIYOIPATA KUPAMBANA NA UMASIKINI

WAHITIMU wa Chuo cha Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA Kampasi ya Mtwara, wametakiwa kutumia elimu waliyopata kwaajili ya kupambana na umasikini kwa ngazi ya mtu mmoja mmoja,jamii inayowazunguka na Taifa kwa ujumla.

Hayo ameyaeleza Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya kwenye Mahafali ya 22 ya Taasisi hiyo ya Uhasibu Tanzania Kampasi ya Mtwara, ambapo jumla ya wanafunzi 408 wamehitimu wakiwemo wanaume 205 na wanawake 203.

Mwaipaya amesema hatua hiyo ya kuhitimu iwe chachu ya kujiimarisha zaidi kitaaluma ili waweze kushindana katika soko la ajira na kujiajiri kwaajili ya kupambana na umasikini.

Aidha Mwaipaya amewataka wadau wa maendeleo kuchangamkia fursa ya uwepo wa chuo hicho kwaajili ya kujenga hosteli ili kukuza pato.

“Tukiangalia kwa asilimia kubwa ya wahitimu wote wanafunzi kutoka mtwara ni wachache sana,tulitaraji kiweza kuona wanafunzi wengi wanatoka hapa kutokana na huduma hii kusogezwa karibu nasi lakini wanafunzi wengi wametoka nje ya Mtwara tutumie fursa hii ambayo serikali yetu imeiona na kutusogezea.”Amesema Mwaipaya

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wizara TIA Nicolaus Shombe amesema serikali kupitia Wizara ya Fedha imetenga jumla ya shilingi bilioni 58.1 kwaajili ya kujenga miundombinu ya kufundishia na kujifunzia katika kampasi za TIA ambapo hatua hiyo imepelekea ongezeko la udahili.

Yusuph Yusuph ni miongoni mwa wanafunzi ambao wamehitimu katika chuo hicho amewataka wahitimu wenzake kutokata tamaa kutokana na changamoto ya ajira iliyopo kwani dunia ya sasa inaamuliwa kwa ubora alionao mtu na kukufikisha unapopataka.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA Kampasi ya Mtwara, wakati wa mahafali ya 22 ya chuo hicho yaliyofanyika leo tarehe 15 Novemba 2024.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Profesa William A. Pallangyo akizungumza na wahitimu wa Chuo cha Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA Kampasi ya Mtwara, wakati wa mahafali ya 22 ya chuo hicho yaliyofanyika leo tarehe 15 Novemba 2024.
Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya akiwa na baadhi ya viongozi wa Chuo cha Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA Kampasi ya Mtwara, wakati wa mahafali ya 22 ya chuo hicho yaliyofanyika leo tarehe 15 Novemba 2024.

Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Taasisi ya Uhasibu Tanzania TIA Kampasi ya Mtwara, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa mahafali ya 22 ya chuo hicho yaliyofanyika leo tarehe 15 Novemba 2024.



Related Posts