Mkurugenzi wa Miradi na Ushirikiano kutoka Camfed Tanzania, Anna Sawaki akizungumza na baadhi ya vyombo vya habari nje ya Kongamano la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC). |
Mkurugenzi wa Miradi na Ushirikiano kutoka Camfed Tanzania, Anna Sawaki (wa kwanza kushoto) akiwasilisha mada kwenye Kongamano la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC). |
Wadau mbalimbali wa elimu wakishiriki katika mijadala kwenye Kongamano la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC) lililofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC). |
Mkurugenzi wa Miradi na Ushirikiano kutoka Camfed Tanzania, Anna Sawaki (kushoto) akishiriki mijadala mbalimbali kwenye Kongamano la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC). |
Na Joachim Mushi, Dar
MRADI wa kuwawezesha Vijana Stadi za Maisha unaoendeshwa na Shirika la Camfed Tanzania umekuwa kivutio katika Kongamano la 4 la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC), uliofanyika jijini Dar es Salaam. Mradi huo unaotekelezwa katika shule takribani 893 ndani ya Halmashauri 35 za mikoa 10 nchini, umewanufaisha vijana wapatao 200,000 kutoka maeneo tofauti.
Akiwasilisha mada kwenye kongamano hilo, Mkurugenzi wa Miradi na Ushirikiano kutoka Camfed Tanzania, Anna Sawaki amesema mradi wa Stadi za Maisha kwa vijana umejaribu kushirikisha jamii pamoja na Serikali katika kuhakikisha watoto wanabaki shuleni na kujifunza ipasavyo, maana unaziangalia changamoto zao na kuzikabili kabla ya madhara kuwa makubwa.
“…Mada niliyowakilisha imejaribu kuwashirikisha wadau wa elimu katika mkutano huu kuangalia miradi yetu inavyoshirikisha jamii yenyewe kutatua changamoto za elimu, tuna program mbalimbali lakini moja ambayo tumeizungumzia zaidi na imewagusa wengi kwenye mkutano huu ni program ya vijana wa kike wanatoka katika jamii zinazowazunguka kurejea kwenye shule zao tena kwa ajili ya kutoa elimu ya Stadi za Maisha. Vijana hawa pia wanatumika kama kiungo cha kuiunganisha jamii husika maana wao ni sehemu ya jamii hiyo,” alieleza akifanya mazungumzo mara baada ya kuwasilisha mada yake, Bi. Sawaki.
“…Wasichana wanaotumika katika mradi huu wa stadi za maisha ni takribani 4200 ambao wanawafahamu vizuri hawa watoto katika jamii husika na wanafahamu mazingira na utamaduni wa jamii hizo, hivyo wananafasi kubwa zaidi ya kushauri hata shule kuhusiana na dalili za mdondoko wa watoto kimahudhurio kwenye shule hizo, endapo wanaona mtoto anadalili za kuacha shule,” anasisitiza akifafanua zaidi programu hiyo.
Aidha aliongeza kuwa wasichana hao wamekuwa wakifanya kazi na viongozi wa vijiji, maofisa kata, maofisa maendeleo ya jamii, na pia maofisa elimu ngazi za halmashauri kwenye maeneo ya mradi, Kwa miaka zaidi ya 10 wamekuwa wakifanya program hiyo ya stadi za maisha kwa kuangazia changamoto mbalimbali ikiwemo upatikanaji wa chakula, upatikanaji wa hosteli kwenye maeneo yenye uhitaji na juzaidi ya wawezeshaji wa . Elimu ya Stadi za Maisha ni zaidi ya vijana 200,000, kutoka shule takribani 893 na Halmashauri 35 na mikoa 10.
Wadau mbalimbali wa elimu wakishiriki katika mijadala kwenye Kongamano la Kimataifa la Elimu Bora (IQEC) lililofanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC). |