RUFAA 5,589 ZA WAGOMBEA ZIMEKUBALIWA : WAZIRI MCHENGERWA

Na Gideon Gregory, Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mohamed Mchengerwa amesema takribani rufaa 16,309 zimepokelewa baada ya muda wa nyongeza wa siku mbili ambapo kati ya hizo rufaa 5,589 zimezokubaliwa.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo Novemba 16,2024 Jijini Dodoma wakati akitoa tathmini ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakao fanyika Novemba 27 mwaka huu kwa wahariri na waandishi wa habari.

“Katika uchaguzi huu nafasi zinazogombewa vyama 18 vya siasa vimeweka wagombea katika nafasi 30,977 kati ya nafasi 80,430 sawa na asilimia 38.51 huku Chama cha Mapinduzi (CCM) kikiweka wagombea katika nafasi zote,”amesema.

Amesema katika nafasi za mwenyekiti wa kijiji zinazogombewa ni 12,280 ambapo vyama hivyo vimeweka wagombea katika nafasi 6,060 sawa na asilimia 49.35.

Aidha ameongeza kuwa nafasi za mwenyekiti wa mtaa zinazogombewa ni 4,264, vyama viliweka wagombea katika nafasi 3,281 sawa na asilimia 76.94 na nafasi za mwenyekiti wa kitongoji zinazogombewa ni 63,886 vyama vimeweka wagombea 21,636 sawa na asilimia 33.87.

Hata hivyo, ametaja baadhi ya sababu zilizosababisha wengine kutoteuliwa ni kukosa sifa ya uraia watanzania, kujidhamini wenyewe, kutojiandikisha kwenye daftari la wapigakura wa serikali za mitaa na wengine kuwa chini ya umri wa miaka 21.

Sanjari na hayo, amesema Ofisi ya Rais – TAMISEMI imefuatilia tuhuma zilizotolewa kwenye maeneo mbalimbali na kubaini hazikuwa na ukweli na zililenga kuleta taharuki na kuchafua mchakato wa uchaguzi unaoendelea vizuri.

Related Posts