TAKUKURU LINDI KUZIDI KUWA MACHO,MAPAMBANO DHIDHI YA RUSHWA KUELEKEA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru Mkoa wa Lindi imeahidi kuendelea kufuatilia kwa ukaribu na kuwachukulia hatua wanachama na viongozi wa vyama vyote vya siasa watakaobainika kujihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu kwenye uchaguzi wa Serikali za mitaa.

Mkuu wa Takukuru Mkoani humo Asha Kwariko ametoa kauli hiyo leo Novemba 16,2024 wakati anazungumza na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari.

Amesema katika uchambuzi wa mifumo yao wamebaini kulikuwepo kwa ukiukwaji wa kanuni na maadili ya uchaguzi katika chaguzi za msingi za ndani ya vyama jambo linalotia mashaka katika kumpata wagombea mwenye sifa.

Aidha amesema taasisi hiyo inawashauri wadau wote kuzingatia kanuni na maadili ya uchaguzi ikiwemo kutii katiba na kuzingatia sheria mbalimbali zinazotumika kuzuia na kupambana na rushwa kwenye uchaguzi.

Ametoa rai kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi kushirikiana na Takukuru katika kuzuia vitendo vya rushwa huku akihimiza wadau muhimu wa uchaguzi kama vyama vya siasa,viongozi wa dini,baraza la wazee,vijana,wanawake na vyombo vya habari kutumia ushawishi wa nafasi walizonazo katika jamii kuhamasisha wananchi washiriki katika kudhibitii rushwa na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27 na uchaguzi Mkuu 2025.

 

 

Related Posts