Ajali mbaya yatokea Geita usiku wa kuamkia leo

Ajali mbaya iliyohusisha Magari Mawili ikiwemo Gari la Abiria (Basi) lenye namba za usajili T. 963 DSR na Gari aina ya Kluger T. 425 DQE zimegongana uso kwa uso katika Kata ya Mponvu , Halmashauri ya Mji Geita na kupelekea Mtu 1 kufariki Dunia na wengine 10 kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo na wengine kujeruhiwa.

Kwa Mjibu wa Mashuhuda waliofika katika eneo la tukio wanasema Dereva mwenye Gari ndogo aina ya Kluger ndio aliyevunja sheria za Barabarani na kupelekea ajari hiyo ambapo kwa Mujibu wa Mashuhuda watu wamejeruhiwa.

Dkt.Thomas Mafulu Mganga Mfawidhi Hospitali ya Halmashauri ya Mji Geita amethibitisha kifo cha Mtu mmoja na wengine 10 kujeruhiwa

Ayo tv inaendelea kulitafta Jeshi la Polisi katika kujua chanzo cha tukio hilo.

 

 

Related Posts