Aliyezushiwa kifo Kariakoo afunguka mbinu walizotumia

Dar es Salaam. Mfanyabiashara Hassan Yahya Mwampamba, ambaye awali alizushiwa kupoteza maisha ndani ya jengo la ghorofa nne lililoporomoka jana Jumamosi Novemba 16, 2024 Kariakoo jijini Dar es Salaam amezungumza na kueleza mbinu alizotumia kujiokoa.

Akizungumza mapema leo Novemba 17, 2024 Hassan amesema: “Mimi kule ndani baada ya jengo kuporomoka tulikuwa watu 26, kwanza tulichagua viongozi kwa ajili ya kudhibiti ile hali sababu watu walikuwa wanalia, baada ya hapo tukatafuta sehemu yenye mwanga tukaitumia hiyo kuanza kuwatoa wenzetu wembamba kisha na sisi tukafuata.

“Nilipofika Muhimbili ndipo nikakuta taarifa kwamba mimi nimefariki, nikawaambia mimi niko hai ila mtandao tu ulikata, na ile picha niliyoituma mtandaoni tuliipiga kama ukumbusho baada ya kuona kuna uhakika wa kutoka, ndipo nikapiga picha yangu mimi peke yangu na nyingine ya watu watatu,” amesema Hassan.

Hassan amefafanua kuwa kati ya watu 26 waliokuwa kule chini wa mwisho ameokolewa leo.

Endelea kuifuatilia Mwananchi…

Related Posts