Beki Simba aeleza kiwango chake

BEKI wa Simba Queens, Ester Mayala amesema siri ya kufanya vizuri msimu huu ni pamoja na maelekezo makubwa ya kocha anapokuwa uwanjani.

Msimu huu beki huyo amekuwa na mwanzo mzuri wa kiwango akicheza mechi nne kwa dakika 360 akiruhusu mabao mawili.

Akizungumzia juu ya kiwango chake, Mayala alisema kocha anamuamini na kumpa nafasi hivyo kama mchezaji kazi yake ni kuipambania timu.

Aliongeza pia kukaa kwenye timu kama Simba kunawapa morali ya kufanya vizuri hata wanapokuwa benchi kutokana na historia ya timu hiyo.

“Tunapambana kwa ajili ya timu na kila tunapopata nafasi tunajitahidi kufanya vizuri, isitoshe kocha wetu anazungumza nasi hadi uwanjani inatupa ukumbusho tunapokosea na kurekebishe,” alisema na kuongeza;

“Sio rahisi kushinda mechi mfululizo, lakini kama timu na wachezaji tunapambana kuhakikisha tunachukua pointi tatu kila mchezo na kuendelea kusalia kileleni.”

Related Posts