Chama la Mtanzania latinga nusu fainali CAF

CHAMA la Mtanzania FC Masar anayoichezea Hasnath Ubamba juzi imetinga husu fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF) kwa kuitandika C.B.E mabao 2-1 nchini Morocco.

Masar inacheza na C.B.E ya Ethiopia iliyopo mkiani mwa msimamo wa kundi B ikiwa haijashinda michezo miwili ikipokea kipigo kutoka kwa Mamelodi Sundown Ladies na Edo Queens inayoongoza kundi hilo kwa tofauti ya mabao ikiwa na pointi sawa na chama hilo la Misri.

Masar ilianza kampeni zake kwa kuitandika Mamelodi bao 1-0 na kuweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuifunga kigogo cha soka la wanawake Afrika huku mtanzania huyo akicheza kwa dakika zote 90.

Mchezo wa pili ilitoka sare ya bila kufungana na Edo na mchezo wa mwisho wa kufuzu nusu fainali ikiitandika C.B.E mabao 2-1 na kuingia hatua hiyo kibabe ikiwa timu pekee haijapoteza mchezo wowote.

Ubamba alianza kwenye mechi zote tatu kwa kumaliza dakika 90 akiwa mtanzania pekee aliyeshiriki michuano hiyo kwa msimu huu.

Masar imeweka rekodi ya klabu ya kwanza ya Misri kufikia hatua ya mtoano kwani Wadi Degla walitolewa katika hatua ya makundi msimu 2021/ 2022.

Kwa matokeo hayo yanaifanya chama la Mtanzania huyo na Edo Queens iliyoitandika Mamelodi Sundown mabao 2-1 kwenye mchezo wa mwisho kucheza nusu fainali.

Timu hizo zimeandika historia kwenye michuano hiyo msimu huu kuitandika bingwa mtetezi Mamelodi na kuitoa hatua za makundi.

Related Posts