Haya hapa majina manusura Kariakoo waliopokelewa Muhimbili

Dar es Salaam. Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), imetoa orodha ya majina 40 ya manusura wa ajali ya jengo la ghorofa kuporomoka Kariakoo waliopelekwa hospitalini hapo kwa matibabu.

Jengo hilo lililoporomoka jana Jumamosi Novemba 16, 2024 asubuhi huku jitihada mbalimbali za uokozi zikiendelea kufanywa kwa uratibu wa Serikali.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha, imesema hadi ilipotimu saa 11 jioni jana, manusura 35 waliruhusiwa kurudi nyumbani.

Hata hivyo, leo asubuhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mpaka jana usiku manusura waliookolewa walikuwa 70 huku waliofariki dunia wakiwa wane.

Related Posts