WIKI iliyopita watahiniwa wa kidato cha nne walianza mitihani ya kumaliza masomo yao, lakini kwa Alliance Girls mambo hayakwenda sawa baada ya kuwakosa nyota wake.
Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha wa Alliance, Ezekiel Chobanka alisema mitihani imewagharimu kwenye mechi mbili ingawa ni lazima vijana wasome na kuendeleza vipaji.
Chobanka alisema aliwakosa takribani wachezaji wanne wa kikosi cha kwanza ambao walikuwa kwenye mitihani yao na kufanya kuwatumia vijana wadogo kwenye mechi.
Aliongeza baadhi wamerejea kikosini na wameanza mazoezi na timu na ambao wanaendelea na mitihani watajiunga na kambi watakapomaliza.
“Wameanza mazoezi na timu kujiundaa na michezo ijayo na sababu ya kupoteza mechi ni pamoja na kuwakosa hao kwa kuwa nilianza nao hawakuwa na uzoefu walikuwa wanacheza kwa vipaji vyao,” alisema Chobanka.
Alliance Girls haiko katika hali nzuri kwani iko nafasi ya tisa ikiwa na pointi moja baada ya sare ya 0-0 na Yanga ikipoteza mechi ntatu zilizosalia.