Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Marynurce Kisozi akitoa maelezo katika mahafali ya 27 ya Chuo hicho.
Mwakilishi wa Mgeni rasmi akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi fani ya uongozaji wa watalii katika mahafali ya 27 ya Chuo cha VETA Mikumi.
Mwakilishi wa Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Denis Londo,Afisa Elimu Sekindari Wilaya ya Kilosa Joseph Kapele akizungumza katika Mahafali ya 27 ya Chuo cha VETA Mikumi.
Mwakilishi wa Mgeni rasmi akipata maelezo kutoka kwa mwanafunzi fani ya uhudumu wa majumbani katika mahafali ya 27 ya Chuo cha VETA Mikumi.
Mwakilishi wa Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Chuo cha VETA Mikumi mara baada ya kuhitimishwa mahafali ya 27 ya Chuo hicho.
Matukio katika picha kwenye mahafali ya 27 ya Chuo cha VETA Mikumi.
*Mkuu wa Chuo aweka mikakati ya mahusiano ya kutanua uwigo ajira kwa wahitimu
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV Mikumi
UFUNDI Stadi ni sekta muhimu kwenye taifa lolote katika kujipatia maendeleo chanya ya kiuchumi kwa ujenzi wa miundombinu pamoja na ujuzi wake kutumika katika viwanda.
Hayo ameyasema Mwakilishi wa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mbunge wa Mikumi Denis Londo,Afisa Elimu Sekondari Wilaya ya Kilosa Joseph Kapele kwenye mahafali ya 27 ya Chuo cha VETA Mikumi, wilayani Kilosa mkoani Morogoro.
Amesema Mataifa mengi yaliyoendelea yamefanikiwa kutokana na kuimarisha sekta ya ufundi katika kuvumbua vitu mbalimbali na kutatua changamoto katika jamii.
Kapele amesema wahitimu wana deni katika taifa kwani walichohitimu kinahitajika sokoni kwenda kukitolea huduma na kuongeza uchumi wao pamoja na Taifa.
Aidha amesema katika shughuli za kila siku au za maisha zinahitaji aina fulani ya stadi za ufundi ya stadi ufundi wa ujenzi wa nyumba,Barabara utengenezaji wa samani,vifaa vya kilimo na mateangenezo ya magari.
Amesema katika maonesho mlioandaa kunaonyesha kuwa ujuzi umeingia wakufunzi wameonyesha uwezo wao kufanya vijana kuwa na sifa zote za kujiajiri na kuajiriwa kwani soko lipo katika pande zote.
Amesema kazi zipo za kutosha kinachotofautisha kwa wahitimu wanaangalia upande wa kuajiriwa lakini serikali imetoa fedha za kukopesha makundi mbalimbali ikiwemo vijana kujiunga katika vikundi.
Kapele amesema elimu na ujuzi wa ufundi katika karne ya 21 inategemea umahiri ,ubunifu ,ari ya utendaji ambapo fundi bora ni yule ambaye anatumia ufundi wake kwa umahiri katika sehemu za kazi pamoja kujifunza kila mnapokutana nayo.
Amesema uchakavu wa miundombinu na vitendea kazi ni baadhi ya chagamoto muhimu lakini pia kunahitaji kwenda sanjari na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia ni moja ni moja ya mambo yanayotakiwa kukabiliana nayo
Kapele amesema Serikali ya awamu ya Sita imepanua uwigo wa vyuo vya ufundi Stadi ili kuwajengea uwezo vijana kupata ajira kwa ajili ya kukuza uchumi.
Nae Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Mashariki John Mwanja amesema amesema kuwa VETA imetengeneza mahusiano na taasisi mbalimbali ikiwemo Magereza kwa wafungwa waliomaliza kifungo waliopata ufundi kupita VETA kwa ajili ya kuwatambua.
Amesema wamekwenda kwa watoa huduma za usafirishaji ikiwemo Bodaboda kupata mafunzo kwa ajili ya kuwatambua.
Aidha amesema jitihada zote ni kwenda katika kuboresha utoaji wa huduma pamoja na kuwa watu wenye ujuzi na wanatambulika kisheria.
Kwa upande wa Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi Marynurce Kazosi kuwa Chuo hicho kina fani 14 ambazo zimeendelea kufanya vizuri na wataongeza fani zingine kutokana na mahitaji yaliyopo sasa.
Amesema kwa mwaka huu 2024 walisajili wanafunzi wa kozi ndefu 605 kwa fani 13 kwa ngazi ya kwanza hadi tatu kwa ngazi ya kwanza 306 ambapo wasichana 142 na ngazi ya tatu 138 kwa fani ya ukarimu na hoteli.
Amesema katika kufikia malengo yenye tija kwa wanafunzi na wahitimu wametengeneza mahususiano kwa watu wa hoteli ,Mbuga za Wanyama kwa ajili ya kupata kupata mafunzo kwa vitendo na matokeo yake ni chanya kwani baadhi yao hupata ajira huko.