Uokozi jengo lililoporomoka Kariakoo waingia siku ya pili

Dar es Salaam. Shughuli za uokoaji zinaendelea asubuhi hii katika jengo la ghorofa lililoanguka Kariakoo jijini Dar es Salaam zikiwa zinaingia siku ya pili tangu tukio hilo litokee.

Asubuhi ya leo Jumapili, Novemba 17, 2024 mtu mwingine ameokolewa, wakati akitolewa kuna mtu amemtambua kwa kumuita jina moja la Michael.

Jengo hilo lililoporomoka jana Jumamosi Novemba 16, 2024 asubuhi, mpaka sasa jitihada mbalimbali za uokozi zinafanyika.

Hata hivyo, mpaka jana usiku, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), ilitoa orodha ya majina 40 ya manusura wa ajali ya hiyo waliopelekwa hospitalini hapo kwa matibabu.

Katika taarifa hiyo iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa hospitali hiyo, Aminiel Aligaesha, inasema hadi ilipotimu saa 11 jioni , manusura 35 waliruhusiwa kurudi nyumbani.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila kwa taarifa aliyoitoa asubuhi ya leo ni kuwa manusura 70 hadi jana waliokolewa huku watu wane wakifariki dunia kutokana na ajali hiyo.

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi

Related Posts