Watu 75 Wameokolewa, zoezi la uokoaji linaendelea kwa ufanisi

NA EMMANUEL MBATILO, MICHUZI TV

Juhudi za Serikali kupitia vikosi mbalimbali katika zoezi la uokoaji wa manusura wa ajali iliyotokea jana Novemba 16,2024 ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa 4,Kariakoo Jijini Dar es Salaam, zimefikia hatua nzuri  ambapo baadhi ya watu walio kwama chini wamefikishiwa maji,glucose pamoja na hewa ya oksijeni,ili kudhibiti madhara makubwa yanayoweza kujitokeza wakati  wanaendelea na zoezi hilo.

Ameyasema hayo leo Novemba 17,2024 Kariakoo -Jijini Dar es Salaam Mkuu Mkoa ,Albert Chalamila akiwa katika zoezi la uokoaji wa manusura wa ajali hiyo.

 RC Chalamila amewatoa hofu wanaosema zoezi la uokoaji linakwenda taratibu  ambapo
uokozi unafanywa kwa kutumia akili na ustadi zaidi ili kutokuleta
madhara zaidi na ndio maana idadi ya wanao okolewa wakiwa hai ni kubwa
zaidi kuliko waliopeza maish

“Kuna watu ambao wako chini tunaowasiliana nao ambapo tumewasihi waendelee kuwa wastahimilivu wakati ambao wataalamu wa uokoaji wanatumia akili kubwa ili jengo zima lisidhurike na kuleta athari kwa watu waliochini”. Amesema RC Chalamila

Aidha Chalamila. amebainisha kuwa hawajaapokea taarifa ya watu waliokufa kutokana na  changamoto ya kupumua isipokua watu waliodhurika ni wale waliopata madhara wakati jengo linaanguka.

Pamoja na hayo Chalamila ameeleza kuwa wamefunga biashara mitaa ya jirani inayozunguka eneo hilo kwa lengo la kupunguza msongamano wa watu ili kurahisisha zoezi hilo la uokoaji.

Amesema taarifa yake ya awali ya uokozi ilionyesha watu 70 walishaokolewa na taarifa ya usiku hadi asubuhi tayari wameshaokolewa 5 na kufanya jumla ya watu 75 hadi kufikia saa moja asubuhi ya leo.

Related Posts