KIRAKA wa Yanga Princess, Wema Maile amesema kama wachezaji hawatamani kupata matokeo wanayopitia sasa hivi na watafanya vizuri mechi zijazo.
Yanga haijaonja ushindi wowote tangu ligi ianze, ikianza sare ya 1-1 na Bunda Queens, 0-0 Alliance, 1-1 na Mashujaa Queens na kupoteza dhidi ya Simba kwa bao 1-0.
Akizungumza juu ya mwenendo wa timu hiyo, Maile alisema kama wachezaji hawatamani kupata matokeo hayo wakiamini watajipanga mechi zilizosalia.
Aliongeza msimu huu umekuwa mgumu kutokana na maandalizi ya kila timu akijipa matumaini bado mapema sana.
“Hatutamani kupata matokeo mabaya, mechi bado ni nyingi tutafanya vizuri, ligi ni ngumu tunapambana kadri ya uwezo wetu bado mechi ni nyingi,” alisema Maile.