Jeshi la polisi Mkoani Morogoro kuchunguza kifo cha Aron

Jeshi la Polisi Mkoani Morogoro linaendelea na uchunguzi wa tukio la Kifo Cha kijana mmoja aliyefahamika Kwa jina la Aron Aron mwenye umri wa miaka 16 mkazi wa Mtaa wa Msimamo kata ya Kihonda Manispaa ya Morogoro baada ya kukutwa akiwa amefariki katika nyumba ambayo haijaisha ujenzi wake( pagale)

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani hapa SACP Alex Mkama amesema taarifa za kupotea kwa kijana huyo ziliripotiwa novemba 16 baada ya kwenda kuchunga mbuzi Kisha kutorejea nyumbani.

Baada ya taarifa hizo Wananchi na Polisi walianza jitihada za kumtafuta ndipo mapema Leo novemba 17 mwili wake umekutwa katika nyumba hiyo huku damu zikitoka masikioni lakini hauna jereha lolote.

Rpc Mkama amesema uchunguzi unaendelea kushirikiana na watalam wa afya Ili kujua chanzo cha kifo chake.

Baba ndogo wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Baraka Kamela amesema Kwa Sasa wanaviachia uchunguzi vyombo vya Usalama kujua chanzo Cha kifo cha ndugu Yao kwani mara zote akienda kuchunga mifugo anarudi nyumbani lakini Siku ya tukio walishangaa hadi usiku hakuweza kurejea

Kwa Sasa mawili umehifahdiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospital ya Rufaa Mkoa Morogoro kwa ajili ya taratibu zingine.

 

 

Related Posts