Kazi za majumbani kwa sasa ni kozi inayotambulika na VETA/ VTA

Mtaalam wa Jinsi ‘Gender Expert’ wa Shirika la Watu Wanajitolea Ulimwenguni Maria Shimba akipunga mikono ya utambulisho kwenye mahafali ya 27 ya Chuo cha VETA Mikumi katika Mahafali hayo Wafanyakazi wa Majumbani walihitimu fani hiyo.

Picha ya Pamoja ya Wahitimu wa fani ya wafanyakazi majumbani ,Wakufuzi pamoja na Mkuu wa Chuo cha VETA Mikumi kwenye Mahafali hicho.

*Zaidi ya wafanyakazi 500 wa majumbani wamehitimu kozi hiyo na kupatiwa vyeti katika kipindi cha 2023 hadi sasa 2024

Na Mwandishi Wetu Shirika la Watu Wanajitolea Ulimwenguni kwa kushirikiana na serikali ya Italia (Italian Agency for Cooperation Development) limesema kuwa lilitoa ufadhili wa kutengeneza mtaala kwa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) na Mamlaka ya Mafunzo ya Amali (VTA) Zanzibar kwa ajili ya wafanyakazi wa Majumbani.

Akizungumza na Michuzi Blog kwenye Mahafali ya 27 ya Chuo cha VETA Mikumi Mtaalam wa Jinsi ‘Gender Expart’ wa Shirika la Watu Wanajitolea Ulimwenguni kwa, Maria Shimba amesema kuwa waliamua kufadhili wafanyakazi wa majumbani kutokana na wafanyakazi hao kutokuwa na weledi wa kazi,unyanyapaa pamoja na kutojua haki zao.

Amesema kuwa baada ya kukamilika kwa mtaala hadi sasa wamenufaika wafanyakazi wa majumbani zaidi ya 500 kwa kusoma katika vyuo vya VETA/ VTA

Maria amesema kuwa vyuo vya VETA na VTA vinavyotoa fani ya wafanyakazi majumbani ni Mikumi ,Dar es Salaam,Iringa ,Dodoma,Lindi ,Tanga na Zanzibar ni Vyuo vya Makunduchi VTA na Mkokotoni VTA pamoja Chuo cha Daya VTA Pemba.

AIdha Maria amesema kuwa wafanyakazi wa majumbani ambao hawajapata kozi ya wafanyakazi majumbani waende na wanaotaka kufanya kazi hiyo waende kusoma fani hiyo katika vyuo hivyo.

Amesema kuwa kwa kusoma kozi hiyo wafanyakazi wa majumbani watakuwa na mikataba ya ajira ya maandishi yenye stahiki zote kwa mujibu sheria za nchi itakayosaidia kupunguza malalamiko kwa pande zote mbili mwajiri na mwajiriwa

“Tunaamini kuwa wafanyakazi wakiwa na mafunzo watakuwa na uelewa utakaosaidia kutatua changamoto zilizokuwa zinawakabili na kuweza kuleta staha ya kazi hiyo”Amesema Maria

Amesema kozi hiyo inatolewa kwa mwezi mmoja,Miezi Mitatu pamoja na miezi sita na wakufuzi wanawapa kile ambacho wanakwenda kufanyia kazi.

Pamoja na mambo mengine Kozi hiyo imejikita katika masomo yafuatayo Food production-Housekeeping &Laundry services,Children & Elderly care, Potential migrant for Dws Life Skills, Reproductive health,Customer care,Labour rights,Resilience

Amesema waajiri ambao wanawafanyakazi ambao hawana fani ya kozi ya majumbani kuwapeleka kusoma itasaidia katika kuboresha utendaji wa kazi.

Related Posts