KOCHA wa Mlandizi Queens, Jamila Hassan amesema bado timu yake haijajipata kutokana na ugumu wa ligi hiyo.
Hadi sasa kwenye mechi nne za ligi Mlandizi haijaambulia ushindi ikipoteza tatu dhidi ya Simba 3-1, JKT Queens 7-0 na Ceasiaa Queens 2-1 na sare moja dhidi ya Get Program.
Kocha huyo alisema bado wanaendelea kujifunza ligi hiyo baada ya kukaa nje kwa takribani misimu miwili wakiangukia ligi ya mkoa.
Aliongeza kuwa licha ya kuendelea kupata somo lakini kikosi chake kina mapungufu eneo la beki ikiruhusu mabao mengi.
“Hatuna madhaifu makubwa lakini eneo kubwa ni eneo la ulinzi ambalo linatusumbua sana tukiruhusu mabao mengi ya ajabu tunaendelea kuwanoa vijana kupunguza makosa hayo,” alisema Jamila.