Marekani yaruhusu makombora yake kutumika dhidi ya Urusi – DW – 18.11.2024

Afisa wa serikali ya Marekani aliyetoa masharti ya kutokutajwa jina amesema Rais Biden ameidhinisha matumizi ya silaha hizo dhidi ya Urusi, suala ambalo limekuwa ombi la muda mrefu la Rais Volodymyr Zelensky.

Awali taarifa hizo zilitolewa na magazeti ya New York Times na Washington Post.  Afisa huyo amesema ruhusa ya matumizi ya silaha hizo ndani ya Ukraine ni jibu kwa hatua ya Korea ya Kaskazini kupeleka wanajeshi wake Urusi katika kuisaidia vitani dhidi ya Ukraine.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky amepongeza uamuzi huo uakisema kuwa, “Mpango wa kuiimarisha Ukraine niliouwasilisha kwa washirika wetu ni wa ushindi. Moja ya mambo muhimu ya mpango huu ni uwezo wa jeshi letu kufika mbali. Leo kuna mengi yanazungumzwa kwenye vyombo vya habari kuhusu sisi kuruhusiwa kuchukua hatua usika. Lakini mashambulizi hayafanywi kwa maneno. Kwa hakika, makombora yatazungumza yenyewe.”

Mbunge wa Urusi Maria Butina amesema ikiwa utawala wa Rais Biden umeidhinisha silaha hizo, utakuwa unahatarisha kutokea kwa vita vya tatu vya dunia.

Kombora la Urusi lawauwa watu 11 Ukraine

Katika hatua nyingine, kombora la Urusi limeripotiwa kuwauwa watu 11 katika mji wa kaskazini mashariki mwa Ukraine wa Summy Jumapili jioni. Watoto wawili wameripotiwa kuwa ni miongoni mwa waliokufa wakati wa shambulio hilo.

Idara ya huduma za dharura ya Ukraine kupitia ukurasa wake wa Telegram imesema kuwa watu wanane na watoto 11 pia wamejeruhiwa.  Shambulio hilo lilifanywa muda mfupi baada ya Urusi kushambulia miundombinumbinu ya umeme katika kile Urusi ilichokiita shambulio kubwa lililohusisha makombora 120 na droni 90. Tukio hilo lilisababisha vifo vya watu wasiopungua 7.

Sumy, Ukraine baada ya mashambulizi ya Urusi 18.11.2024
Shambulio la anga lililofanywa na Urusi katika mji wa Sumy UkrainePicha: State Emergency Service of Ukraine in Sumy region/Handout/REUTERS

Soma zaidi: Mashambulizi ya Urusi dhidi ya Ukraine yawaua watu kadhaa na kuharibu miundombinu

Wakati huohuo, Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limedai kuwa Urusi inahusika katika kampeni inayoendelea ya uhalifu dhidi ya watu na watoto wa Ukraine.

Shirika hilo limesema limethibitisha mashambulizi 17 yaliyosababisha watoto kuathiriwa kwa mwaka 2024 pekee.  Mtafiti wa shirika hilo anayehusika na UkrainePatrick Thompson  ametoa wito kwa wahusika wa vitendo hivyo vilivyo kinyume cha sheria kuwajibishwa kisheria

 

 

Related Posts