Dar es Salaam. Miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya ghorofa lililoporomoka Kariakoo, inaagwa leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Hadi jana usiku ililiripotiwa watu 13 wamepoteza maisha katika ajali hiyo iliyotokea juzi huku 84 wakijeruhiwa.
Akizungumza na Mwananchi, Mwenyekiti wa kamati ya maafa, William Lukuvi amesema tayari utambuzi wa miili hiyo umefanyika.
Amesema baada ya utambuzi, leo Jumatatu Novemba 18, 2024 miili hiyo itaagwa katika tukio litakaloongozwa na Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa.
Endelea kufuatilia Mwananchi.