PPRA na FDH wawapa darasa la matumizi ya mfumo wa Nest wenye ulemavu zaidi ya 200 Dodoma

Watu wenye ulemavu zaidi ya 200 wamepatiwa mafunzo ya sheria ya manunuzi na fursa zilizopo kwa makundi maalum na matumizi ya mfumo wa Nest ya PPRA ili wanufaike na asilimia 30 ya fedha za bajeti ya serikali zinazotengwa kwa makundi hayo kwaajili ya manunuzi ya umma.

 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na wenye ulemavu Ridhiwani Kikwete akiwa amewakirishwa na Mkurugenzi wa Idara ya watu wenye Ulemavu Ofisi ya Waziri Mkuu Rashid Maftaha katika warsha ya kujengea uwezo watu wenye ulemavu Jijini Dodoma.

 

Kikwete amesema serikali imewezesha PPRA kuwezesha makundi maalum mbalimbali ikiwemo kundi la watu wenye ulemavu kwa kuwajengea uwezo wa manunuzi ya umma ambapo asilimia 30 zimetengwa mahususi kwaajili ya makundi maalum ambapo asilimia kumi ni maalumu kwa wenye ulemavu.

 

Alisema pia kundi hilo linawezesha kiuchumi kwa kupatiwa ajira ili waweze hata kuajiri waondokane na umasikini ambapo sheria imeagiza kutoa ajira asilimia 3 ya ajira kwaajili ya watu wenye ulemavu ambapo zaidi ya watu wenye ulemavu 200 wameajiriwa katika nyanja mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na idara ya elimu, ustawi wa jamii, afya na watu wa lishe.

Aidha Kikwete alisema Ofisi ya Waziri Mkuu imeanza mchakato wa kupitia Sera ya watu wenye ulemavu ya mwaka 2004 ambapo hatua mbalimbali imeshafanyika ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini na kwasasa wapo katika rasimu ya Sera hiyo ambayo ipo katika hatua mbalimbali iwasilishwe.

“Lengo la kuandaa sera hii ni pamoja na kuhakikisha tunahimalisha uchumi wa mmoja mmoja makundi ya jamii nzima ya watu wenye ulemavu kwa kupitia asilimia 30 ya fedha za manunuz ya umma ambazo zimetengwa mahususi kwa makundi maalumu ikiwemo watu wenye ulemavu” alisema.

Alisema pia zipo fursa nyingine za uwezeshaji kiuchumi ambayo ni mikoo ya asilimia 10 inayotokana na mapato ya halmashauri ambapo asilmia 2 imetengwa kwaajili ya watu wenye ulemavu ili wajikwamue kiuchumi ili aendelee kuishi maisha ya staha na kuweza kuchangia kwenye uchumi wa taifa.

Alisema Warsha hiyo imewajengea uelewa wa asilimia 30 ya fedha za umma zinapaswa kutengwa kwa mujibu wa sheria kwaajili ya makundi maalum katika zabuni za umma kwaajili ya makundi hayo wakiwemo watu wenye ulemavu.

“Nendeni mkachangamkie hiyo fursa ili muweze kujikwamua kiuchumi” alisema Kikwete.

Aidha aliwapongeza FDH kwa kuwahudumia watu wenye ulemavu na kusimamia utekelezaji kwa kuhakikisha Ofisi ya Waziri mkuu inaendelea kutekeleza sera, sheria na miongozo mbalimbali katika ngazi ya mamlaka ya serikali za mitaa.

Hatahivyo Kikwete ametoa wito kwa taasisi zingine kuungana na PPRA kutoa eliu ya kufundisha fursa zilizopo katika sheria zao zinazohusu wenye ulemavu katika taasisi zao ili waweze kuzinadi wenye ulemavu waweze kuzijua wanufaike na fursa hizo.

Mkurgenzi wa Taasisi ya Foundation for Disabilities FDH Michael Salali amesema warsha hiyo imehusisha watu wenye ulemavu zaidi ya 200 wakiwemo wenye ualbino, wasioona, walemavu wa viungo, wasiosikia na wenye ulemavu wa akili.

Hatahivyo aliwashukuru PPRA kwa kutoa kipaumbele katika kujengea uwezo kundi la watu wenye ulemavu kwa mafunzo hayo ili waje kujiajiri na kuajir waondokane na umasikini.

Mkurugenzi Mkuu wamamlakamya udhibiti wa manunuzi wa Umma PPRA CPA Salmini Malole alisema katika Mwaka wa Fedha uliopita, yaani tangu Julai 1, 2023 hadi Juni 30, 2024, kwa ujumla, vikundi 85 vya vijana vilipata zabuni zenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni Tatu na Milioni Mia Tisa.

Katika Mwaka huu wa fedha pia, zabuni zimeendelea kutolewa kwa makundi maalum, ambapo zabuni za zaidi ya Shilingi Bilioni Moja na Milioni Mia Nane zimetolewa kwa vikundi 39. Kati ya vikundi hivyo, vikundi vya vijana ni 29, vikundi vya wanawake ni 29 na wazee ni kikundi kimoja.’

‘Tunaamini, kutokana na jitihada hizi za kuwajengea uwezo zinazoendelea pamoja na mwamko waliouonesha, kundi la watu wenye ulemavu litakuwa sehemu ya watakaopata zabuni kupitia Mfumo wa NeST yaani Kundi hili la watu wenye ulemavu, katika zile asilimia 30 zilizotengwa wao wametengewa Asilimia 10’

‘Hivyo tunawahamasisha watu wenye ulemavu nchini kuchangamkia fursa kwenye huu upendeleo maalum uliotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita, na umewekwa kisheria’ alisema CPA Malole.

Naye Afisa Mahusiano wa FDH Furahini Chemakaa ametaja changamoto zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini kuwa ni pamoja na baadhi ya wakuu wa taasisi ya umma na binafsi kutowaelewa watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na kutokujua lugha ya alama hali inayopelekea huduma kwa watu wenye ulemavu kukwama.

Aliongeza kuwa changamoto nyingine ni kutotekelezwa sheria namba Tisa ya mwaka 2010 hasa kwenye eneo la ajira ambayo inamtaka kila mwajiri anapotangaza nafasi za ajira anatakawa kutenga asilimia 3 kwaajili ya watu wenye ulemavu.

Mwenyekiti wa Bodi ya FDH Dr. Henry Humba ameishukuru serikali kwa kuendelea kuwesha watu wenye ulemavu wameendelea kuwezeshwa kiuchumi ili wajikwamue kiuchumi na kuchangia maendeleo ya jamii na taifa.

Alisema Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Ofisi ya Waziri Mkuu amehakikisha watu wenye ulemavu wamewezeshwa kiuchumi ili waweze kuchangia kwenye maendeleo ya wenyewe na taifa kwa ujumla.

 

Related Posts