Na Oscar Assenga, Pangani
Waziri wa maji Jumaa Aweso amemuagiza mkandarasi anajenga mradi wa maji wa miji 28 kuhakikisha unakamilika kabla ya wakati Ili kuwaondolea wananchi adha ya ukosefu wa maji.
Maagizo hayo ameyatoa wilayani Pangani wakati alipotembelea ujenzi wa matenki ya kuhifadhi maji katika eneo la Madanga na kimang’a
” Huu mradi fedha zake zipo tayari hivyo nimtake mkandarasi aongeze nguvu kazi Ili uweze kukamilika kabla ya wakati wake na wananchi waweze kupata huduma karibu na maeneo yao”amesema Waziri Aweso.
Mradi wa maji wa miji 28 unatekelezwa katika wilaya nne za mkoa wa Tanga ambapo msimamizi wa mradi huo Mhandisi Yohana Mgaza amesema kuwa mradi huo mpaka Sasa umefikia asilimia 60.
“Mradi unatarajiwa kujenga matanki ya kuhifadhi maji nane na tayari bomba zimeshalazwa umbali wa zaidi ya km 107 kati ya 188 yanayohitajika”amesema Mgaza.
Mradi wa maji wa miji 28 ulitikiwa ukamilike mnamo mwezi Disemba mwaka 2025 hata hivyo unatarajiwa kukamilika mwezi wa sita mwakani huku ukiwa tayari umefikia asilimia 60