Na Jane Edward,Arusha.
Wataalamu wa ununuzi na ugavi kutoka halmashauri za Mkoa wa Arusha wamekutana Jijini Arusha katika semina ya siku mbili ya kuwajengea uwezo Wataalamu wa ununuzi na ugavi kujifunza sheria mpya ya manunuzi na namna gani ya kuchakata zabuni kupitia mfumo wa Nesti.
Akifungua mafunzo hayo Katibu tawala Mkoa wa Arusha Mussa Misaille,amesema ni vyema kila mtaalamu akafanya kazi kwa weledi na kwamba mafunzo hayo yawasaidie Pindi wanapokuja kukaguliwa.