WATAALAM WA MANUNUZI NA UGAVI JIEPUSHENI NA VITENDO VYA RUSHWA

Vero Ignatus,Arusha
 

“Tumefanya ukaguzi hapa Mkoani Arusha na tumegundua changamoto kubwa ya baadhi ya wafanyakazi kwenye vitengo vya ununuzi hawajasajiliwa jambo ambaloni uvunjaji wa sheria kwa Makusudi kwani sheria inaeleza wazi kuwa ni marufuku kufanyakazi kama huhasajiliwa tunawaomba Sana changamoto hiyo iishe”

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi nchini(PSPTB)Godfred Mbanyi ametoa wito kwa vitengo vya ununuzi na ugavi kuzingatia sheria kanuni na taratibu za manunuzi katika kutekeleza majukumu yao huku akiwataka wale wote ambao hawajasajiliwa na bodi kujisajili haraka iwezekanavyo.

Wito huo ameutoa leo Novemba 19,2024 Jijini Arusha akizungumza wataalamu wa manunuzi na Ugavi( PSPTB)kwa kushirikiana na wataalam wa sekta za halmashauri zote na sektetarieti za Mkoa wa Arusha ambapo alisema yeyote anayefanya kazi bila kusajiliwa anavunja sheria za nchi.

“Nasisitiza kuzingatia sheria kanuni na taratibu za manunuzi katika kutekeleza majukumu yenu,na nawataka wale wote ambao hawajasajiliwa na bodi kujisajili haraka iwezekanavyo kwani iko kwa mujibu wa sheria na anayefanya kazi bila kusajiliwa anavunja sheria za nchi”alisema Mbanyi

Aidha Mbanyi amesema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wataalamu hao juu ya sheria mpya ya ununuzi na namna ya kusimamia mikataba,pqmoja na kuzingatia yaleyote watakayojifunza ili wakitoka waende kuyatekeleze kwa vitedo

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Missaile Musa aliwataka wataalam wa ununuzi na Ugavi nchini kuwa waadilifu na weledi katika utendaji kazi wao huku wakitanguliza uzalendo pamoja na kuzingatia kanuni na taratibu wakati wa kutekeleza majukumu yao.

Missile amewataka kuzingatia misingi ya taaluma yao kwani taaluma hiyo ya ununuzi na Ugavi ni kubwa hivyo lazima waitendee haki kwa kufuata maadili ya kazi hiyo na kuweza kuwa mfano wa kuigwa,huku akiwataka kujiepusha na vitendo vya rushwa na kujikita zaidi katika kusimamia kikamilifu fedha zote za umma zinazotengwa kwa ajili ya miradi mbalimbali.

Catherine Mwamasage ni Mkuu wa kitengo cha manunuzi kutoka TANAPA,vilevile ni mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo amepongeza PSPTB kwa kuwapatia mafunzo hayo na kusema kuwa yatawasaidia kupata maarifa zaidi na wataenda kuyafanyia kazi kwa vitendo.
 

Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya wataalamu wa ununuzi na ugavi hapa nchini(PSPTB)Godfred Mbanyi  akizungumza kwenye semina hiyo inayoendelea mkoani Arusha leo Novemba 2024
 

Katibu Tawala wa Mkoa wa Arusha,Missaile Musa akizungumza  wakati akifungua mafunzo kwa wataalamu wa manunuzi na Ugavi  mkoani Arusha leo Novemba 19,2024


 

Baadhi ya washiriki wakiwa kwenye semina inayoendelea mkoani Arusha leo Novemba 2024 mafunzo kwa wataalamu wa manunuzi na Ugavi  mkoani Arusha leo Novemba 19,2024

Related Posts