Katibu mkuu wa jumuiya ya umoja wa vijana azindua kampeni za uchaguzi Pwani

Katibu mkuu wa jumuiya ya umoja wa vijana ya chama cha mapinduzi Jokate Mwegelo siku ya leo amezindua rasmi kampeini za uchaguzi wa serikali za mitaa katika mkoa wa pwani ambapo shughuli za uzinduzi wa kampeni hizo zimefanyika katika wilaya ya kibiti mkoani Pwani.

Mbali na yote aliyoyazungumza Jokate huku akiwaomba wanachama wa chama hicho kuwapigia kura viongozi mbali mbali wa chama hicho kwa maendeleo ya vijiji na vitongoji vyao.

Pia Jokate ameweza kuwapokea jumla ya wanachama 20 kutoka vyama vingine na kuhamia CCM ambao wamerudisha kadi za vyama vyao ikiwemo baadhi ya wagombea wa vyama hivyo na kuwakabidhi rasmi kadi za CCM na kuwarasmisha kama wana CCM.

 

Related Posts