Mr Manguruwe na Mkaguzi wake waendelea kusota rumande baada ya kukosa dhamana

Mfanyabiashra, Simon Mkondya (40) maarufu kama Manguruwe na Mkaguzi, Rweyemamu John (59) wanaendelea kusota rumande kutokana na kukosa dhamana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Manguruwe ambaye Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla International Ltd na mwenzake walifikishwa mahakamani hapo Novemba 5, 2024 akikabilia na mashtaka 28 ikiwemo utakatishai fedha wa Shilingi Milioni 92.2.

Wakili wa Serikali, Winniwa Kasala amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu , Anna Magutu kwamba kesi hiyo ilikuja kwa ajili ya kutajwa, upelelezi bado haujakamilika hivyo anaomba tarehe nyingine ya kutajwa.

Kesi hiyo iliahirishwa hadi Desemba 4, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Inadaiwa washtakiwa hao walijipatia Sh92.2 milioni kutoka kwa watu 19 ambao walitoa kiasi tofauti cha fedha baada ya kuahidiwa kuwa watapata faida mara mbili hadi tatu ya fedha walizotoa.

Related Posts