Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dokta Samia Suluhu Hassan ameizawadia Taifa Stars Sh700 milioni kama pongezi baada ya timu hiyo kufuzu Afcon 2025 itakayofanyika mwakani nchini Morocco.
Stars imefuzu kwenye mashindano hayo Kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuitandika Guinea bao 1-0, lililofungwa na Simon Msuva dakika ya 61.
Akizungumza kwa niaba ya Rais Samia, Waziri wa Utamadini Sanaa na Michezo, Dokta Damas Ndumbaro amesema zawadi hiyo imetolewa kwa kuthamini kupambana kwao hadi kufuzu, na tayari pesa hizo zimeingizwa kwenye akaunti ya Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo.
Pia Stars imepewa mualiko wa kutembelea Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwezi Februari mwakani.