Taswa yaipongeza TFF kufuzu kwa Stars AFCON

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) kimetoa pongezi kwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kaimu Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Hemed Suleiman ‘Morocco’, wasaidizi wake na wachezaji wa Taifa Stars kwa kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwaka 2025 nchini Morocco.

Stars iliifunga Guinea 1-0 katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam na kukata tiketi hiyo.

Kaimu Katibu Mkuu wa Taswa Imani Makongoro amesema hatua hiyo ni muhimu sana katika maendeleo ya michezo hapa nchini.

“Tunawapongeza wananchi pia waliofurika katika uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya kuiunga mkono Taifa Stars kwa dhati na kuwapa hamasa wachezaji wetu mwanzo hadi mwisho wa mchezo mgumu na kupata ushindi,” amesema Makongoro. Novemba 19, 2024.

Makongoro ametoa wito kwa Watanzania kuendelea kuiunga mkono Taifa Stars ili iendelee kufanya vizuri zaidi kimataifa na kupeperusha vema bendera ya nchi.

“Tunaishukuru sana Serikali ya Rais Samia kwa sapoti kubwa inayoitoa katika sekta ya michezo mbalimbali hapa nchini ukiwemo soka’ na kuleta hamasa ya maendeleo,”

“Ni vizuri hamasa hii inaendelea ili timu zetu ziendelee kufanya vizuri zaidi kimataifa,” amesema.

Ametoa wito wa kuanzamatayarisho mapema kwa fainali za mwakani kwa sababu ushindani wa fainali hizo ni mkubwa.

Related Posts