Vodacom yazindua Vodashop katika stesheni ya SGR Dodoma kuwasogezea huduma wateja

Vodacom Tanzania Plc imezindua duka lake jipya
(Vodashop) katika stesheni ya SGR iliyopo mkoani Dodoma huku ikiwa na mpango wa
kufungua duka lingine mkoani Morogoro. Hatua hii muhimu inaonyesha dhamira ya kampuni
hiyo kutoa huduma stahiki kwa wateja wake huku wakipanua wigo wa upatikanaji kote
nchini. Hii ikiwa ni muendelezo wa mikakati yake ya kuhakikisha wateja wake
wanapata huduma haraka pale wanapohitaji.

Ikiwa imepangwa kimkakati kuhudumia abiria wa reli
ya SGR, maduka haya mapya, pamoja na la Dar es Salaam, yatakuwa vituo
vinavyotoa huduma zote za kampuni hiyo. 
Wasafiri
sasa wanaweza kupata huduma za M-Pesa, simu janja ana vifaa vyake Pamoja na msaada
wa wataalam watoa huduma kwa wateja kwa urahisi, ili kuhakikisha wanaunganishwa
na mtandao muda wote wa safari zao.

Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Mwenyekiti
wa bodi ya wakurugenzi Vodacom Plc, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo  alisisitiza
umuhimu wa hatua hii, “tunafuraha kuzindua Vodashops hizi zilizoko ndani
ya stesheni ya SGR hapa jijini Dodoma na baadae Morogoro ikiwa ni hatua muhimu
katika kuwasogezea wateja wetu huduma bora. Tukitambua mchango wa SGR katika
ukuaji wa uchumi wetu, tumejiandaa kutoa huduama stahiki kwa watumiaji wake. Aidha, uzinduzi huu ni sehemu ya maono yetu mapana ya  kuipeleka Tanzania kwenye ulimwengu wa
kidigitali
kwa kuhakiisha tunawaunganisha watanzania wengi kwenye mtandao.”

Madukahaya mapya yatatoa huduma ya viwango vya juu,
yakirahisisha upatikanaji wa bidhaa na huduma mbalimbali za kampuni hiyo.
Upanuzi huu unaendana na maono ya Vodacom ya kukuza ujumuishwaji wa kidijitali,
kuimarisha muunganisho na kusaidia ukuaji wa kijamii na kiuchumi kote nchini.

“Napenda kutoa pongezi za dhati kwa timu
ya Vodacom kwa uzinduzi wa duka la Vodashop katika stesheni yetu ya SGR Dodoma.
Huu ni mfano bora wa juhudi za kampuni hii katika kuboresha upatikanaji wa
huduma kwa Watanzania, hasa wale wanaposafiri. Tunapongeza Vodacom kwa
kuendelea kuwa mshirika katika maendeleo ya taifa ya kiuchumi. Wameendelea kuwekeza
katika miundombinu ya kisasa inayosaidia kukuza uchumi na kuimarisha
muunganisho wa taifa letu. Hatua hii ni muhimu katika kuhakikisha kila
Mtanzania anafikiwa na huduma bora popote alipo”, aliongea Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary S. Senyamule.

Uzinduzi wa SGR Vodashop unathibitisha ahadi
za Vodacom za kutoa huduma bora kwa wateja wakati wote pamoja na suluhisho za
kibunifu na zenye kuzingatia mahitaji ya wateja ili kuboresha maisha ya
Watanzania. Wakati nchi inakumbatia mabadiliko ya kidijitali, Vodacom Tanzania
inabaki kuwa taasisi yenye nguvu inayohakikisha kila mteja anaunganishwa katika
mawasiliano kwa urahisi zaidi, na haswa  hasa kwa wale walio safarini.

Kwa upande wake Mkuu wa Kanda ya Kati, Joseph
Sayi alidokeza, “Tunatambua kuwa wateja wetu pia wanategemea sana njia za
kidijitali ili kuweza kujihudumia wenyewe popote walipo,iwe ni kupitia aplikesheni
ya Vodacom, M-Pesa Super App, tovuti yetu au mitandao ya kijamii, wateja wetu
wanaweza kuwasiliana nasi wakati wowote, mahali popote. Tumejidhatiti kutoa
huduma ndani ya maduka na mtandaoni ili kuhakikisha kuwa wateja wetu hawapati
changamoto yeyote wakati wa matumizi ya huduma zetu,”.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule (katikati) akikata utepe kuashiria kufungua rasmi duka la Vodacom  lililopo eneo la kituo cha  mwendokasi (SGR)  cha  Samia Jijini Dodoma leo. Kulia ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Vodacom Tanzania ,Jaji Mstaafu Thomas Mihayo na kushoto ni Mdau wa Vodacom ,Emmanuel Makaki .



 

Related Posts