*Kupiga,Kutuma SMS pamoja na Data hakuna kuweka mawazo.
Na Mwandishi Wetu Shirika la mawasiliano Tanzania TTCL limeshusha neema kwa wananchi katika ununuaji wa vifurushi katika Msimu wa Sikuu za mwisho wa mwaka kupitia kampeni yake ya Waletee.
Kampeni hiyo ni maboresho ya kampeni iliyopita na utofauti wake kupata virushi unavyovitaka na sio kulazimshwa.
Maboresho hayo ni makubwa kwa watumiaji wa simu za mkononi kwa kufanya watanzania wote Bara na Zanzibar kupata huduma mahali popote walipo bila vikwazo vyovyote ikiwemo ukomo wa matumizi ya vifurushi pamoja na kiwango cha pesa ikiwa ni kuwapa fursa ya kuwasiliana kuelekea msimu wa sikukuu.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini dar es salaam mkurugenzi wa Biashara TTCL Vedastus Mwita amesema Mawasiliano ni chachu kubwa ya biashara mtandaoni ambayo inahitaji kutumia huduma hiyo kwa gharama nafuu pamoja na kupata vifurushi ambavyo vitatumika mpaka mwisho badala ya kupewa muda maalum wa matumizi na kufanya kukimbia katika kufanya maongezi au ujumbe mfupi pamoja data.
Amesema kupiga simu ,kutuma Sms pamoja na data hakuna mawazo ni kutumia bila kikomo na bila mawazo ya kuchukuliwa kifurushi.
Mwita amesema Katika kuhakikisha watanzania wanapata huduma hizo TTCL imekuja na kampeni ya walete nyumbani mambo ni moto ikilenga zaidi kuwaleta watanzania kutumia hudum za TTCL maeneo makuu matatu huduma za data, kurahisisha na kuboresha huduma za sauti na kupata muda wa maongezi bila kuwa na kikwazo cha muda wa matumizi na pesa.
Vifurushi hivyo ni Bufee Tena, Jiachie Extra pamoja Data ambavyo vifurushi hivyo vitakwenda hadi mwaka.
Katika Kampeni hiyo TTCL imemtambulisha Baba Levo kuwa mshirika na Balozi wa Kampeni ya Waletee nyumbani.
Baba Levo amesema kuwa katika ubalozi wake atautendea haki katika kuwafikia wananchi na kutumia huduma za Mawasiliano za TTCL
Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Vedastus Mwita akimkabidhi kitendea Balozi wa TTCL Baba Levo kwa ajili ya kutangaza kampeni ya mwisho wa mwaka ya Waletee kwa ajili ya watazania kupata huduma za mawasiliano ya bei ya Chini.
Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Vedastus Mwita akikata utepe akiwa na Balozi wa TTCL Baba Levo kuashiria uzinduzi wa kampeni ya mwisho wa mwaka ya Waletee kwa ajili ya watazania kupata huduma za mawasiliano ya bei ya Chini.
Mkurugenzi wa Biashara wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL, Vedastus Mwita akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na kampeni ya mwisho wa mwaka ya Waletee kwa ajili ya watazania kupata huduma za mawasiliano ya bei ya Chini.