WAZIRI MKUU AZINDUA KAMATI UCHUNGUZI KUPOROMOKA KWA JENGO KARIAKOO

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amezindua Kamati ya Wataalamu ya Uchunguzi wa Jengo lililoporomoka katika eneo la Kariakoo ikiwa ni utekelezaji wa maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuchunguza chanzo cha tukio hilo pamoja na kufahamu ubora na uimara wa majengo yote yaliyoko Kariakoo.

Tarehe 16 Novemba, 2024, majira ya saa 3 asubuhi, ilitokea ajali ya kuporomoka kwa jengo la takriban gorofa tatu lililopo mtaa wa Agrey Kata ya Kariakoo, Jijini Dar es Salaam na kusababisha athari kubwa kwa watu na mali katika eneo hilo.


Related Posts