CCM KIBAHA MJI YATEMA CHECHE ZAKE YAWANADI WAGOMBEA WAO KWA KISHINDO

NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani Ndg. Kitte Mfilinge amezindua rasmi kampeni za wagombea wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini na kuwataka kuhakikisha wanaungana na kuwa na umoja kwa lengo la kuweza kushinda katika mitaa yote kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Katibu huyo ameyabainisha hayo wakati wa uzinduzi huo uliofanyika katika viwanja vya kwa mbonde mjini kibaha na kuwakutanisha wagombea wa CCM wanaowania katika nafasi mbali mbali ikiwemo nafasi ya wenyekiti wa serikali za mitaa kutoka mitaa yote 73 na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa chama wa ngazi za Wilaya, Mkoa pamoja na jumuiya zake mbali mbali.

Aidha aliongeza kwamba chama cha mapinduzi kimefanya uzinduzi huo kwa lengo kubwa la kuwanadi wagombea mbali mbali walioteuliwa kwa ajili ya kuwania nafasi mbali mbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo nia na madhumuni ni kuhakikisha CCM inashinda kwa kishindo bila kupoteza hata mtaa mmoja.

“Ngugu zangu wana ccm leo tumekuja kwa lengo la kuwanadi wagombea wetu mbali mbali ambao watashiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa lakini cha msingi inapaswa kuhakikisha tunachagua viongozi wenye sifa wanaotokana na chama chetu ambao wataweza kuleta mabadiliko makubwa kwa wananchi katika suala zima la kufikisha huduma muhimu na maendeleo kwa wananchi,”alisema Katibu huyo.

Pia aliongeza kuwa chama cha mapinduzi kinahitaji mtu ambaye atakwenda kutimiza wajibu wake kwa kuibuka kero na kusikiliza chanagamoto mbali mbali kutoka kwa wananchi na kuzifanyia kazi na kuzipeleka katika kamati za kata za maendeleo ili ziweze kufikishwa katika viongozi wa halmashauri na hatimaye serikali iweze kuzifanyia ufumbuzi.

Katika hatua nyingine hakusita kuwasisitizia wenyeviti wote wa serikali za mitaa kupitia chama cha mapinduzi ambao watachaguliwa wanapaswa kuhakikisha wanakwenda kutekeleza ilani ya chama kwa vitendo na kutekeleza yale mambo mbali mbali ambayo yamefanya katika miradi mbali mbali ya maendeleo na yale ambao yametajwa kwenye ilani na bado hayajafanyiwa kazi wanapaswa kuyaendeleza.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka amesema kwamba wamejipanga vilivyo kwa ajili ya kwendakushiriki kikamilifu katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa ambapo matarajio yao makubwa ni kushinda katika mitaa yote kupitia wagombea wa chama cha mapinduzi (CCM)

Koka alisema pia amewahimiza wanachama wa ccm pamoja na wananchi kwa ujumla kuweza kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi huo wa serikali za mtaa kwa lengo la kuweza kuwachagua wagombea wa CCM ili waweze kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huo na kuwaletea wananchi chachu ya maendeleo katika nyanja mbali mbali.
Aidha Mbunge Koka aliwapongeza wagombea wote ambapo wameweza kuteuliwa na CCM katika kugombea katika nafasi mabali mbali na kuwahimiza kuhakikisha pindi watakapochaguliwa kuendelea kusimamia utekelezaji wa ilani ya chama ikiwemo katika kuwaletea maendeleo wananchi.

Naye Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamaka alisema kwamba mwenendo mzima wa mchakato wa kura za maoni tayari umeshamalizika hivyo wanachama wote na viongozi waliochaguliwa kuungana kwa pamoja ili kuelekeza nguvu zote katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kushinda kwa kishindo katika mitaa yote.

Mwenyekiti Nyamka aliongeza kuwa Rais wa awamu wa sita Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya mambo makubwa katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo hivyo wanachama wote wa CCM pamoja na wananchi wanapaswa kumuunga mkono na kwenda kuwachagua wagombea wote kwa kishindo katika uchaguzi huo ili waweze kuendelea kutatua kero na changamoto za wananchi.

 

Related Posts