DART yatoa safari nne za bure kwa wataonunua kadi

Na Mwandishi Wetu

Wakala wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) imesema kuwa katika msimu wa siku kuu za mwisho wa mwaka wanatoa sh.30000 kwa safari Nne kwa watakaonunua kadi kwa ajili ya kutumia katika safari za mabasi yaendayo haraka.

Hayo amesyasema Mtendaji Mkuu wa DART Dkt.Athuman Kihamia wakati akizungumza na waandishi habari kuhusiana na matumizi ya kadi kwa ajili ya mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa baada ya kufanya safari hizo kadi walizonunua wataendelea kuziwekea fedha katika kuendelea kutumia huduma hiyo.

Dkt.Kihamia amesema kuwa matumizi ya kutumia kadi ni suluhisho ya kudhibiti fedha ya serikali.

Aidha amesema kuwa wananchi watumie kadi hizo pamoja na wale ambao hawana wachukue kukutana na ofa hiyo.

“Tunataka wananchi waweke fedha katika kadi kwani inarahisisha kujua matumizi ya safari katika mabasi yaendayo haraka”Amsema Dkt. Kihamia.

Aidha amesema moja ya juhudi ya serikali katika utumiaji huo ni pamoja na kuhakikisha wananchi hawachafui mazingira kutokana na kuwa mfumo tiketi za karatasi.
 

Mtendaji Mkuu wa DART Dkt.Athumani Kihamia akizngumza na waandishi wa Habari  kuhusiana na ofa ya safari nne wataonunua kadi za mabasi yaendayo haraka ,jijini Dar es Salaam.

Related Posts