JUMBE ATANGAZA KUNUNUA KILA GOLI LA STAND UNITED SH. LAKI 2

Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa, akipiga Penalti wakati akizindua mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama “DR. SAMIA – JUMBE CUP’  hivi karibuni

Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa, akipiga Penalti wakati akizindua mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama “DR. SAMIA – JUMBE CUP’ hivi karibuni

Mdau wa mchezo wa mpira wa miguu, Mhandisi James Jumbe Wiswa, akipiga Penalti wakati akizindua  mashindano ya Ligi ya Taifa Ngazi ya Wilaya ya Shinyanga, yanayojulikana kama “DR. SAMIA – JUMBE CUP’ hivi karibuni

 

 Na Mwandishi wetu – Shinyanga

 

Katika hatua ya kuimarisha michezo na kutoa motisha kwa wachezaji wa soka, Mhandisi James Jumbe ametangaza kutoa zawadi ya shilingi laki mbili (200,000) kwa kila goli linalofungwa na timu ya Stand United  ‘Chama la Wana’ katika mechi za mashindano. 

 

Akitangaza mpango huo, Mhandisi Jumbe amesema “Michezo ni njia muhimu ya kuleta umoja na pia ni chanzo cha ajira kwa vijana wetu. Ni furaha yangu kutoa mchango huu na kuendelea kuunga mkono jitihada za Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kukuza michezo nchini.”

 

 

“Nimechukua maamuzi haya ikiwa ni kuunga mkono mkakati wa Rais  Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuendeleza michezo nchini, unaojulikana kama GOLI LA MAMA, ambapo jamii ya Shinyanga inashirikiana kwa karibu katika kukuza michezo na kutoa fursa kwa vijana”,amesema.

 

 

Mhandisi Jumbe amesisitiza kuwa kiwango cha fedha kitakachotolewa kinaweza kuongezeka kulingana na ufanisi wa timu hiyo, huku akitoa wito kwa mashabiki wa soka na wanajamii kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika michezo na kuunga mkono juhudi hizi za maendeleo ya michezo.

 

Amesema ataendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha michezo inaendelea kuwa na nafasi muhimu katika jamii, huku akihimiza wanajamii kujitokeza kwa wingi kuunga mkono timu za soka za mkoa wa Shinyanga.

 

 

Mhandisi Jumbe, ambaye ni mpenzi mkubwa wa michezo na pia mtendaji wa maendeleo, ameonyesha dhamira ya dhati katika kukuza michezo, hasa soka, ambapo amewahakikishia wachezaji wa timu ya Stand United motisha ya kifedha kwa kila goli watakalofunga. 

Hatua hii inakuja wakati ambapo timu ya Stand United inajipanga kuonyesha kiwango cha juu cha mchezo katika mashindano yajayo, huku wachezaji na viongozi wa timu wakisema kuwa motisha hii itawaongezea nguvu ya kufanya vizuri zaidi.

Stand United inatarajiwa kuongeza juhudi na ufanisi katika mashindano kutokana na mchango huu wa kifedha.

 

Huu ni mfano mzuri wa ushirikiano kati ya viongozi, wanamichezo na jamii katika kukuza na kuendeleza michezo, na Shinyanga inaendelea kuwa kitovu cha maendeleo ya michezo nchini.

Related Posts